BWAWA LA KUOGELEA LAMUAMISHA ZLATAN HOTEL YA MAN UTD NA KUHAMIA HOTELI YA MAN CITY
Zlatan Ibrahimovic anaamini msema kweli ni kipenzi cha Mungu.
Ndiyo
maana akaamua kuihama hotel ya Lowry ambayo hutumiwa zaidi na timu ya
Manchester United na kuhamia Radisson Blu ambayo hutumiwa zaidi na
kikosi cha Man City.
Uamuzi wake wa kuhama hotel aliyopangiwa wakati anatafutiwa nyumba ni kwamba haina bwawa la kuogelea.
![]() |
| BWAWA LA KUOGELEA LA HOTELI YA RADISSON |
Yeye
alikuwa anaishi katika hoteli hiyo pamoja na familia yake. Huku
wakiendelea kusubiri wapate nyumba wanayotaka na zoezi la madalali
linaendelea.
Lakini
akaona hakuna hata bwawa la kuogelea na familia yake inalihitaji. Hivyo
hakuwa na zaidi ya kusema anahamia katika hoteli yenye bwawa la
kuogelea bila ya kujali kwamba Man City huwa wakiishi hapo au vyovyote
vile.



Post a Comment