Wanamuziki, Vanessa
Mdee na mpenzi wake Juma Jux ‘Jux’ baada ya manenomaneno kuzagaa kuwa
wameachana juzikati wapenzi hao walionekana kwenye mbuga ya wanyama ya
Serengeti iliyopo mkoani Mara kisha kwenda kula bata kwenye hoteli ya
bei mbaya ya Singita.

Akipiga
stori na safu hii juzi akiwa Serengeti, Vanessa alisema kuwa, wameamua
kwenda huko kwa mapumziko ya siku nne ikiwa ni sehemu ya kufanya utalii
wa ndani na wamekula bata za kutosha.

“Ni
mambo ya utalii wa ndani, tumekuja huku kupumzika kidogo, siyo lazima
kwenda nchi za nje kwa mapumziko, humuhumu Bongo kuna sehemu unakwenda
na unajisikia furaha,” alisema mwanadada huyo.
Singita ni hoteli ya kifahari iliyopo mkoani Mara ambayo inaiingizia nchi fedha nyingi za kigeni.

Post a Comment