Faiza, Wema ndani ya bifu nzito kisa Idris!
Faiza Ali.
MTIFUANO wa maneno makali
umeibuka kati ya wasanii wa fi lamu Bongo, Wema Sepetu na Faiza Ali
chanzo kikiwa ni Faiza kuposti maneno ya ‘kumdis’ Wema kutokana na mfumo
wake wa maisha ya kimapenzi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza
aliandika kuwa Wema anapenda sana ‘ving’asti’ (dogodogo) akitolea mfano
Idris Sultan aliyekuwa mpenzi wake, kisha akasema kuwa anaomba Mungu
asije akapata mtoto wa kiume atakayependa ku-date na wanawake waliomzidi
umri.
Kutokana na maneno hayo yaliyojaa shari
ndani yake, Ijumaa lilimtafuta Wema kuzungumzia posti hiyo ambapo
alipopatikana alikuwa na haya ya kusema: “Yaani mimi simpendi kabisa
yule binti, namuona ni mpumba** tu, ndiyo maana hata Sugu akaona si
mwanamke anayefaa kuwa mkewe. Hana akili kabisa.”

Post a Comment