SAMATTA AISOGEZA KRC GENK EUROPA CUP, APIGA BAO LA PILI DHIDI YA PODGORICA
Mbwana
Samatta amefunga bao moja na kuiwezesha KRC Genk ya Ubelgiji kushinda
kwa mabao 2-0 dhidi ya Buducnost Podgorica katika mechi ya kuwania
kucheza Europa Cup. Genk ilikuwa nyumbani.
Samatta
alifunga bao hilo katika dakika ya 79, baada ya Kebano kuwa amefunga la
kwanza katika dakika ya 17 kwa mkwaju wa penalti.
Samatta
aliunganisha vizuri krosi ya Kebano na kufunga bao hilo la pili muhimu
dhidi ya timu hiyo kutoka Montenegro. Ushindi ni muhimu kwa kuwa ni sawa
na kikosi cha Genk kinaongoza kwa mabao 2-0.
VIKOSI:
KRC Genk
: Bizot, Castagne, Dewaest, Kumordzi, Uronen, Ndidi, Buyens (73
'Heynen) Kebano (76' Karelis), Bailey, Buffalo and Samatta (87
'Trossard).
Buducnost Podgorica
: Dragojevic, Vusurovic (84 'Camaj), Mitrovic, Vukcevic, Radunović,
Pejakovic (74' Seratlic) Raickovic (59 'Janketić), Hoko, Đalović,
Mirkovic, Raspopovic

Post a Comment