Pombe kali zitamuua Wolper huku akidaiwa kupewa mimba na mpenzi wake Harmonize!
Dar es Salaam: Msanii ‘hot’ wa
filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anaonekana kubobea kwenye
unywaji wa pombe kali huku kukiwa na madai kuwa, mpenzi wake, Rajabu
Abdulhan ‘Harmonize’ amemtundika mimba, jambo ambalo ni hatari kwa afya
yake.
Hilo limekuja kufuatia juzikati staa
huyo kunaswa tena akiwa anakunywa pombe iliyodaiwa ni kali alipokuwa
kwenye Shoo ya Black Tie iliyofanyika kwenye Ukumbi wa King Solomoni,
Namanga jijini Dar. CHANZO: GPL
Watu wa karibu wa staa huyo wanaeleza
kuwa, mara nyingi wamekuwa wakimuona mdada huyo akiwa anakunywa pombe
kali, hali ambayo inaweza kuwa ni hatari kwa maisha yake.
“Yaani Wolper pombe anazokunywa
zitammaliza, sijui kama anaweza kupitisha siku bila kunywa na mbaya
zaidi sasa anagida zile pombe kalikali, kwa kweli namsikitikia sana,”
alisema rafiki wa karibu wa staa huyo aliyeomba hifadhi ya jina.
“Mbaya zaidi kuna hizi taarifa kuwa ana
mimba, sasa ikiwa hivyo ni wazi yanaweza yakamkuta kama yaliyompata
shosti wake Wema Sepetu (Wema inadaiwa kutumia pombe kali ni moja za
sababu ya mimba yake kutoka).”
Akizungumzia unywaji wa pombe wa Wolper
huku ikidaiwa ni mjamzito, dokta mmoja wa hospitali ya serikali iliyopo
jijini Dar aliyetambulisha kwa jina moja na Dokta Makere alisema:
“Iko hivi, matumizi ya pombe kwa
wajawazito husababisha watoto kuzaliwa wakiwa na uwezo mdogo wa akili
(mataahira) lakini pia pombe inaweza kuharibu mimba na kusababisha itoke
kabla hivyo ni vyema akina mama wawe makini na hilo.”
“Hapa usione hivi, nimeanzia mbali ni muendelezo tu na wala sioni shida,” alisema Wolper huku akionekana ‘kapendeza’ ile mbaya.
Alipoulizwa kwa nini anapigia ‘tungi’
wakati inadaiwa ana mimba, staa huyo alionekana kutompatiliza paparazi
wetu na kumtaka amuache afanye yake.

Post a Comment