Ukawa Waziba Midomo Kwa Karatasi, Watoka Bungeni
Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia akizungumza na wanahabari nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma.
WABUNE wa Kambi ya rasmi ya
Upinzani Bungeni, leo wameibuka na mtindo wa aina yake ndani ya Ukumbi
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mjini Dodoma, baada ya
kuamua kuziba midomo yao kwa kugundisha karatasi na plasta kisha kutoka
nje ya ukumbi huo ikiwa ni adhima ya kueleza hisia zao za kutosikilizwa
mapendekezo yao na Naibu Spika, Mh. Dkt. Tulia Ackson.
Hali ya wabunge wa Kambi ya Upinzani
walianza kutoka nje ya bunge hilo yapata wiki ya pili mfululizo kutokana
na kile walichokitangaza kuwa, hawatahudhuria kikao chochote cha bunge
hilo kitakachoongozwa na Naibu Spika Dkt. Tulia kwa
kuwa amekuwa akiwanyima wapinzani nafasi ya kutoa maoni yao bungeni
hivyo kuminya haki yao ya msingi ya ikiwa wao ni wawakilishi wa
wananchi.
Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia
amesema wameamua kutumia mtindo huo mpya kwa sababu Bunge limekataa
kusikiliza hoja na mapendekezo yao ndani ya bunge hilo.






Post a Comment