Simba wamchongea Kessy kwa Pluijm
Beki mpya wa Yanga, Hassan Kessy.
Wilbert Molandi, Dar es SalaamWAKIWA kwenye maandalizi ya mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe, beki mpya wa Yanga, Hassan Kessy amewekwa kitimoto na kocha wake Mholanzi, Hans van Der Pluijm kwa siku mbili. Beki huyo, hivi sasa yupo kwenye mgogoro na uongozi wa Simba ukidai mchezaji huyo ni mali yao bado huku mwenyewe akisema mkataba wake umemalizika tangu Juni 15, mwaka huu. Sakata hilo, lilianza wakati timu hiyo ilipopanga kumtumia nyota huyo kwenye mechi na MO Bejaia ya Algeria wakati beki wao Juma Abdul akiwa nje ya uwanja akiuguza majeraha ya
enka.
Aliongeza kuwa, kikao kingine walikifanya na kocha huyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya mazoezi ya asubuhi siku moja kabla ya mechi
na TP Mazembe, ambapo anasema alitumia dakika tano kumwelezea kwa undani na akamuelewa, hivyo akashangaa kuona Simba wakimuwekea ngumu.
“Leo (jana) meneja wangu na Chama cha Wachezaji Tanzania (Sputanza) wakiwa na mkataba wangu wataelekea TFF kwa ajili ya kwenda kuishtaki Simba wanaodai kuwa mimi ni mali yao. “Hilo suala ni ndogo sana, lakini wenyewe wanataka kulifanya kuona kubwa, ninaamini hilo litamalizika hivi karibuni baada ya meneja wangu na Sputanza kulifikisha TFF ili ukweli upatikane.
“Nakosa furaha kwenye timu yangu mpya ya Yanga na mimi ninataka kucheza na kitu kikubwa kinachonichanganya, kocha mwenyewe anaonekana kutaka kunitumia, lakini inashindikana kutokana na hali hiyo, nimefanya naye kikao mara mbili akihoji mkataba wangu akitaka kujua ukweli,”alisema Kessy.
CHANZO: CHAMPIONI

Post a Comment