Pam D aahidiwa darasa la Hip Hop na R.O.M.A
MKALI wa Miondoko ya Hip Hop,
Ibrahim Musa ‘R.O.M.A’ amefunguka atampa darasa la Hip Hop, staa wa
Bongo Fleva, Pam D ili aweze kuchana mistari kama afanyavyo yeye.
Akipiga stori na safu hii, R.O.M.A
alisema mdada huyo amekuwa akitaka awe mchanaji mzuri hivyo ameamua
kumfundisha ili wawe wanakamua pamoja kwenye shoo mbalimbali kwani
anahisi ana damu ya Hip Hop.
“Niko karibu sana na Pam, nimepanga
kumfundisha kuchana ili awe kama mimi kwani najua anaweza. Kwa mfano
Julai 7, mwaka huu tutapanda jukwaa moja kule Ngonga Beach Resort pande
za Mbeya pamoja na akina Mesen, Kadja Nito na Msami Baby. Kolabo yangu
na yeye itanogaje siku hiyo!” alisema R.O.M.A ambaye siku za hivi
karibuni amekuwa ‘klozi’ na mwanadada huyo.

Post a Comment