KOCHA MPYA SIMBA HUYU HAPA, ANATOKEA GHANA, ALIWAHI KUIFUNDISHA TIMU YA TAIFA YA RWANDA

Kocha mpya wa Simba ni Sellas Tetteh Teivi, raia wa Ghana, pia ni mmoja wa makocha maarufu barani Afrika.
Kwa
sasa kocha huyo gwiji barani Afrika, ndiye kocha mkuu wa timu ya taifa
ya Sierra Leone na Simba imefanya mazungumzo naye kwa takriban wiki
nzima, imefahamika.
Tayari
Simba imetenga dau, tayari imefanya mazungumzo naye na yenyewe
imeshakubali kila kitu, kilichokuwa kinasubiriwa ni kitu kimoja tu, neno
“Yes” kutoka kwa Tetteh.
Kocha
huyo aliyewahi kuinoa timu ya taifa ya Ghana, ni maarufu kutokana na
mambo kadhaa likiwemo lile la kuiongoza timu ya vijana wa Ghana chini ya
miaka 23 kucheza Kombe la Dunia mwaka 2013.
Pia
aliwahi kuwa kocha wa muda wa timu kubwa ya taifa ya Ghana na wakati
akiwa mwanasoka, alicheza kwa mafanikio katika klabu za Great Mao Mao,
Zebi na Hearts of Oak kwao Ghana, pia nchini Nigeria alipozitumikia ACB,
Julius Bereger na Iwuanyanwu.
Habari za uhakika kutoka nchini Ghana kwa rafiki wa karibu wa kocha huyo, zimethibitisha Simba kufanya naye mazungumzo.
“Mazungumzo
yao yamefikia pazuri sana, kocha alichelewa kutoka Sierra Leone ndiyo
ikawa shida. Lakini leo (jana) atawapa Simba jibu rasmi, mwanzo alitaka
kuona ‘profile’ ya Simba.
“Simba wenyewe wamemwambia wanasubiri na leo (jana) ni mwisho, la sivyo wataendelea na plani nyingine,” kilieleza chanzo.
Alipoulizwa Mwenyekiti wa Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe kuhusiana na hilo, alionekana kuwa mkali hiyo jana.
“Nafikiri
si sahihi kusema vitu nusunusu, tuacheni tumalize kama kweli ni huyo au
mwingine mtajua. Sipendi kuzungumzia vitu nusunusu,” alisema Hans Poppe
ambaye amekuwa akipambana kuhakikisha Simba inarejea kwenye fomu.
Iwapo
Tetteh atachelewa, uhakika kabisa Simba itaenda kwenye mpango C
kumyakua kocha wa zamani wa Azam FC, Joseph Omog raia wa Cameroon.
Mpango A ulikuwa ni Kocha Kallisto Pasuwa wa Zimbabwe ambaye amesitisha
kuja baada ya timu yake kufuzu Caf.
CHANZO: SALEH JEMBE
CHANZO: SALEH JEMBE
Post a Comment