KESHO TFF KUIKUBALIA YANGA IFANYE UCHAGUZI WAKE, ITATOA VISINGIZO HIVI..
RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI |
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linatarajia kukutana na seretarieti ya Yanga, kesho.
Taarifa
zinaeleza, TFF haitakuwa na ujanja zaidi ya kuiruhusu Yanga ifanye
uchaguzi wake tofauti na ilivyokuwa ikishikilia msimamo wake kupitia
kamati ya uchaguzi.
Yanga imekuwa ikiomaa kutaka kufanya uchaguzi wake kwa kuwa ni kwa mujibu wa katiba ya Yanga.
Lakini TFF imekuwa ikisisitiza ina haki ya kufanya hivyo, jambo ambalo linaonekana kukosa mashiko.
Tayari
Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ametangaza Rais wa TFF, Jamal Malinzi
atazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na suala hilo.
Lakini
habari za uhakika zinaeleza Malinzi, atatangaza kuwapa nafasi Yanga
kufanya uchaguzi wao kwa kufuata utaratibu ambao ni sahihi.
TFF
itatoa mikono yake na kuipa Yanga imalize jambo hilo na huenda suala la
“Yanga iko katika michuano ya kimataifa”, ndiyo litakuwa neno la TFF
kutaka kuipa Yanga nafasi iendelee na uchaguzi wake.
Wakati
uamuzi huo wa TFF unaibuka, bado kuna tuhuma nzito kwa shirikisho hilo
kwamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya TFF, Alloyce Komba
na viongozi wa BMT wanatuhumiwa kutaka kumng’oa Mwenyekiti wa Yanga,
Yusuf Manji na msaidizi wake Clement Sanga.
Tayari
Yanga imewasilisha malalamiko yake kuhusiana na suala hilo kwa Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Kati ya viambatanisho ni
mkanda ambao una sauti zinazoelezwa kuwa ni za wahusika wakipanga namna
ya kumg’oa Manji kwa figisu.
Post a Comment