Kajala Amwanika Bwana Mpya!!
Staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja
Bwana mpya wa Kajala Masanja.
DAR ES SALAAM: Baada ya kuwa
kimya kwa muda mrefu, staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja juzikati
alimwanika bwana’ke mpya, kufuatia kupigana kibuti na Mbongo Fleva,
Quick Raca, Risasi linakujuza.
Katika Pool Party ya staa mwenzao,
Shilole, iliyofanyika katika uwanja wa ofisi ya BKT iliyopo Masaki
jijini Dar es Salaam, Kajala alimtambulisha mwanaume huyo bila kumtaja
jina, akisema ndiye mtu wake rasmi kwa sasa.
“Naona unanitolea macho na kunitamani
muda mrefu na unavyopenda umbeya unataka kujua hawa nilionao ni kina
nani, naomba ufahamu kuwa huyu ndiye mchumba wangu wa sasa, ndiyo maana
unaniona niko naye,” alisema msanii huyo.
Kajala, ambaye pia alimuonya bwana’ke
huyo kuwa makini na paparazi wetu, alithibitisha usemi huo baada ya
kuondoka pamoja na mtu wake huyo katika viwanja hivyo kuelekea Coco
Beach kabla ya baadaye kuonekana tena pamoja wakinywa kinywaji kimoja
ndani ya Ukumbi wa Club Billicanas.
Kabla ya kuwa pamoja na Quick Raca,
Kajala alikuwa na mumewe, Faraji Chambo ambaye alihukumiwa kifungo cha
miaka saba gerezani, Machi 2013 baada ya kupatikana na hatia ya
utakatishaji pesa, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu.
CHANZO: GPL
CHANZO: GPL
Post a Comment