Chozi la Mobeto laana kwa Lulu!
Kufuatia staa wa filamu
za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kudaiwa kumpora mwanaume aliyezaa
naye, chozi la mwanamitindo anayeuza nyago kwenye video za wasanii wa
Bongo Fleva, Hamisa Hassan Mobeto linaelezwa kuwa ni laana tosha kwa
mwigizaji huyo.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Mobeto,
mrembo huyo ambaye ni sura ya mauzo kwenye matangazo ya nguo za kike,
amekuwa akimwaga chozi kila kukicha huku lawama zote akizielekeza kwa
Lulu.
Chanzo hicho kilidai kuwa, Mobeto
amekuwa akilalamika kwamba, Lulu alijua fika mwanaume huyo ni mzazi
mwenzake lakini akamchukulia na kumsababishia maumivu ya kutelekezewa
mtoto wa kike aliyezaa na jamaa huyo mwaka jana.
“Kiukweli chozi la Hamisa (Mobeto) kila
kukicha ni laana tosha kwa Lulu. Unajua hakuna kitu kibaya kwa mwanamke
kama kuporwa mwanaume wake waziwazi na kuachiwa majukumu ya mtoto huku
adui ukimjua.
“Kibaya zaidi ni tambo za Lulu
mitandaoni. Kitendo cha Lulu kutamba na mwanaume huyo kinamuumiza sana
Mobeto kwa sababu naye ni mwanadamu. Ana moyo wa nyama kama Lulu.
“Pia ukiacha tambo, Lulu amekuwa
akisababisha mtoto wa Mobeto anatukanwa jambo lililomuongezea machungu
kwani mtoto ni malaika ambaye hajui chochote lakini amekuwa
akiunganishwa kwenye ugomvi huo,” kilieleza chanzo hicho.
Alipotafutwa Mobeto hivi karibuni
kuhusiana na sakata hilo, hakuwa tayari kumzungumzia Lulu na mwanaume
huyo lakini akaweka wazi kwamba kinachomuumiza ni mwanaye kuhusishwa na
ugomvi huo.
“Ishu ya Lulu na …(anamtaja mwanaume)
siwezi kuizungumzia, kitu ambacho kinaniumiza ni kumwingiza mwanangu
kwenye haya mambo. Mtoto wangu anakuwa anajumlishwa katika mambo ambayo
hayamuhusu kabisa na hakupaswa kuhusishwa,” alinukuliwa Mobeto na
kuongeza:
“Hakuna mzazi ambaye angekubali mwanaye
aongelewe kwenye mambo yasiyo mazuri. Ningekuwa sina mtoto wala
nisingeumia lakini kwa sababu kuna mtoto ambaye hana hatia wala hajui
kinachoendelea hivyo sipendi na naumia sana.”
Jitihada za kumpata Lulu ziligonga
mwamba baada ya simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa
ujumbe mfupi wa SMS na chatting za WhatsApp hakujibu.
Ishu hiyo ya laana kwa Lulu ilipigiliwa
msumari na mama wa marehemu Steven Kanumba alipozungumza na wanahabari
wetu hivi karibuni katika futari iliyoandaliwa na mwigizaji Illuminata
Poshi ‘Dotnata’, nyumbani kwake, Ubungo jijini Dar.
Alisema Lulu analiliwa na wanawake wengi
kwani wapo ambao alikuwa na uhusiano na waume zao wakafariki dunia huku
wengine wakiachwa na watoto wadogo na kubaki wakilea wenyewe.
“Lulu ana machozi ya wanawake wengi,
Mungu anaona na ninaamini machozi hayo hayataenda bure ipo siku atakuja
kuvuna anachopanda kwa sasa,” alisema mama Kanumba pasipo kutaja
wahusika moja kwa moja.

Post a Comment