CAF YAMPITISHA KESSY NA WAPYA WOTE YANGA KUCHEZA KOMBE LA SHIRIKISHO
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO
la Soka Afrika (CAF), limepitisha majina ya wachezaji wanne wapya wa
Yanga, kipa Benno David Kakolanya, Hassan Hamisi Ramadhan ‘Kessy’,
Vincent Andrew Chikupe na Juma Hassan Mahadhi kucheza Kombe la
Shirikisho.
Yanga
inafungua dimba na Mouloudia Olympique Bejaia Juni 19, mwaka huu,
Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria na sasa wanne hao wako
huru kucheza.
Yanga
ambayo imeweka kambi katika hoteli ya Rui mjini Antalya, Uturuki tangu
Jumapili na itaondoka kesho kwenda Bejaia kwa ajili ya mchezo huo
unaosubiriwa kwa hamu.
Ofisa
Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas Mapunda
ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba wametumiwa leseni za
wachezaji hao kutoka CAF.
“CAF
imetuma leseni za wachezaji hao wanne wapya wa Yanga na maana yake sasa
wako huru kucheza Kombe la Shirikisho,”amesema Mapunda.
Kakolanya
amesajiliwa kutoka Prisons ya Mbeya, wakati Kessy ametoka kwa mahasimu,
Simba, Vincent ametoka Mtibwa Sugar na Mahadhi ametoka Coastal Union.
Mechi
hiyo itachezeshwa na marefa wa Morocco, Bouchaib El Ahrach
atakayepuliza kipyenga akisaidiwa na washika vibendera, Redouane Achik
na Youssef Mabrouk.
Baada
ya mchezo huo, Yanga itarejea Dar es Salaam kuwakaribisha mabingwa wa
Afrika, TP Mazembe Juni 28 katika mchezo wake wa pili wa Kundi A.
Na
katika mchezo huo, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limechanganya marefa
kutoka nchi tatu tofauti, ambao ni Janny Sikazwe wa Zambia
atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano
Dos Santos wa Angola na Berhe O'michael wa Eritrea.
Timu
nyingine katika Kundi A ni Medeama ya Ghana ambayo itafungua dimba na
TP Mazembe mjini Lubumbashi Juni 17, mwaka huu, mchezo ambao
utachezeshwa na marefa wa Shelisheli Bernard Camille, Hensley Danny
Petrousse na Eldrick Adelaide.
Kikosi kamili cha Yanga kilichopo kambini Uturuki ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benno Kakolanya.
Mabeki;
Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Mbuyu
Twite, Kevin Yondan, Pato Ngonyani, Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' na
Bossou anayetarajiwa kufika leo.
Viungo; Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke na Godfrey Mwashiuya.
Washambuliaji; Donald Ngoma, Matheo Anthony na Amissi Tambwe.
Msafara
upo chini ya Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm, Kocha Msaidizi
Juma Mwambusi, Kocha wa makipa, Juma Pondamali, Daktari Edward Bavu,
Mchua Misuli, Jacob Onyango, Mtunza Vifaa Mohammed Mpogolo na Meneja
Hafidh Saleh.
![]() |
| Hassan Kessy (kushoto), Juma Mahadhi (katikati) wakiwa na Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh wakati wa safari ya Uturuki |
CHANZO: BIN ZUBEIRY BLOG

Post a Comment