AKILIMALI AIBUKA NA MAPYA, ATAJA SABABU TATU ZA TFF KUIHUJUMU YANGA
Katibu
Mkuu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali ameibuka na kusema
kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linapaswa kubadilishwa jina na
kubadikwa lile la ushabiki wa TP Mazembe.
Akilimali
amesema pamoja na kelele nyingi za TFF kutaka kuonyesha Yanga haijui
sheria lakini kuna njama za kila aina zimekuwa zikifanywa kutaka
kuiangusha Yanga.
Kiongozi
huyo wa wazee wa Yanga ameishutumu TFF kuingia kwenye mtandao wa Caf na
kupanga tarehe bila kuiambia Yanga halafu ikatangaza kwamba Yanga
walichelewa.
“Yanga
walichelewa? Kama TFF ni ya Tanzania vipi haikuzungumza na Yanga na
kuwaeleza hilo? Hapa kuna kitu cha ajabu kabisa, TFF wanaweza vipi
kupanga tarehe bwana halafu waseme Caf.
“Tena
Yanga ilitaka mechi ichezwe baada ya watu kufuturu. Lakini kwa kuwa
wanajua muda huo, kwenye TV kutakuwa na taarifa ya habari, basi wakaamua
kuipangia Yanga icheze mchana.
“Sasa
hapa unaangalia maslahi ya Yanga au ya TV. Kweli hii si haki na hiki
ndiyo chanzo cha TFF kuihujumu Yanga kwa kuwa inataka watu wengine
wafaidike,” alisema Akilimali na kuongeza.
“Wanasema
Caf ndiyo wana haki ya matangazo ya TV, sawa. TBC wana uwezo pia, vipi
hawakutoa nafasi, huenda wangeweza kulipa fedha nyingi zaidi kwa Caf.
“Kwa nini wamelazimisha Azam tu, TBC ina vifaa na Wachina wamewapa vifaa vipya kabisa hivi karibuni.
“Najua watu wanawaona Yanga kama hawajui, wanawaona kama vile wanapayuka. Lakini ndani yake hawajui kuna nini.
“Nashangazwa
sana na TFF wanavyofanya, wanashindwa kuthamini mchango wa Yanga
kufikia hapa ilipo. Ndiyo inayowafanya TFF sasa wawe busy kuwasiliana na
Caf na wanasikika kimataifa.
“Kwani
lini mara ya mwisho timu ya Tanzania kucheza hatua hii. Hawa TFF vipi
wanaonekana kama hawakufurahishwa na Yanga kufika hapo,” alihoji
Akilimali.
Yanga imekuwa katika malumbano makubwa na TFF huku ikidai shirikisho hilo limekuwa likifanya mambo bila ya kufuata utaratibu.
Lakini
TFF imekuwa ikisisitiza kuwa Yanga hawakujifunza mambo mengi sana ikiwa
ni pamoja na kutokwenda kwenye semina ya Caf wakati wa upangaji ratiba.
Lakini
kuhusiana na hilo, Akilimali anasema: “Hao TFF nimesikia nao walitakiwa
kwenda kwenye semina pia hawakwenda. Sasa kwa upande wa Yanga
wanshupalia kwelikweli. Kawaulize, vipi hawakwenda kwenye semina, huenda
nao kuna mambo mengi hawajui.”
Post a Comment