Vodacom Tanzania yazindua mtandao wa 4G wenye kasi zaidi
Uzinduzi huo umefanyika kwenye ukumbi
wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa
ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Akiongea kwenye uzinduzi huo,
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema kuwa spidi ya mtandao
wa 4G wa Vodacom haina tofauti na ile inayopatikana kwenye nchi zilizoendelea.
Alisema kuwa mtandao huo utatumika kama
chachu ya maendeleo kwenye sekta nyingi nchini.
“4G kwetu sio teknolojia, 4G kwetu ni
kiwezeshaji, ni kiwezeshaji kwa serikali, kiwezeshaji kwa biashara, ni
kiwezeshaji kwa watumiaji wetu,” alisema. “Inachofanya inafungua fursa mpya,
uwezekano mpya,” aliongeza.















Post a Comment