TFF YAAMUA KUWEKA MGUU WAKE SUALA LA VURUGU WALIZOFANYIWA YANGA ANGOLA
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limesema litafanyia uchunguzi tuhuma za Yanga
kufanyiwa vurugu nchini Angola ilipokuwa ikicheza na Sagrada Esperanca
mechi ya kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.
Yanga
imelalamika kufanyiwa vurugu hizo tangu ilipotua nchini humo katika Jiji
la Luanda hadi ilipokuwa mjini Dundo, ambapo walihangaishwa katika
usafiri na kuibiwa baadhi ya vifaa vyao.
Pia
maofisa wa Esperanca waliwazuia waandishi wa habari wa Tanzania kufanya
kazi zao ipasavyo ikiwemo kuwakataza kupiga picha na kuketi sehemu
zisizostahili kwa kazi zao.
Hata
hivyo, Yanga ilifungwa bao 1-0 na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi
Kombe la Shirikisho kwani katika mchezo wa awali jijini Dar es Salaam
ilishinda mabao 2-0. Imefuzu kwa mabao 2-1.
Katibu
Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, amesema watakaa na kujadili kile
kilichotokea Angola kisha watafanya uchunguzi na kuchukua hatua.
“Kama
shirikisho hatukufurahishwa na vitendo walivyofanyiwa Yanga, pia
nichukue nafasi hii kuwapongeza kufuatia hatua waliyoifikia,” alisema
Mwesigwa.
“Tutakaa na kufanya uchunguzi wa kina juu ya walichofanyiwa Yanga, tukibaini tatizo tutajua tuchukue uamuzi gani juu ya hilo.”
Post a Comment