RONALDO ARUSHA JIWE GIZANI MADRID IKILIONYESHA KOMBE LA UBINGWA ULAYA KWA MASHABIKI WAKE
Mshambuliaji
wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amerusha kombora kwa wapinzani wake
na kusema wanamuonea wivu lakini atabaki kuwa namba moja.
Hata
hivyo, Ronaldo ambaye alifunga penalti ta mwisho wakati Madrid
ikiishinda Atletico Madrid na kubeba kombe hilo kwa penalti 5-3,
hakueleza moja kwa moja anamlenga nani.
Ronaldo
ameyasema hayo wakati wa hafla ya mashabiki wa Madrid kulipokea kombe
la ubingwa wa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Ronaldo sasa ameshinda kombe hilo mara tatu pia ametwaa tuzo tatu za mwanasoka wa dunia.
Raia huyo wa Ureno ameendelea kusisitiza ataendelea kubaki namba moja miongoni mwa wanasoka bora kwa kipindi hiki.







Post a Comment