KAMATI YA NIDHAMU TFF YASHINDWA KUWAJADILI NGOMA, TAMBWE, BOCCO
Kikao
cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
kinafanyika kesho Jumanne Mei 3, 2016 kwenye ukumbi wa ofisi za
shirikisho zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es
Salaam.
Kikao
hicho cha kupitia mashauri mbalimbali yaliyowasilishwa TFF, ilikuwa
kifanyike Jumapili Mei Mosi, lakini kiliahirishwa kwa sababu ya wajumbe
wengi walikuwa na udhuru.
Wadau
watakaojadiliwa kesho ni pamoja na Kocha Mkuu wa Azam FC ya Dar es
Salaam, Stewart Hall na wachezaji wake wakiwamo John Bocco, Shomari
Kapombe, Aishi Manula na Kipre Tchetche.
Wengine
ni nyota wa Young Africans SC ya Dar es Salaam ambao ni Amissi Tambwe
na Donald Ngoma wakati kutoka timu ya JKT Rwakoma ya Mara wamo Paulo
Jinga, Zephlyn Laurian na Idrisa Mohamed.
Wengine
ni Ismail Nkulo, Said Juma, Idd Selaman na Edward Amos wa Polisi
Dodoma, kadhalika Abel Katunda wa Transit Camp ya Dar es Salaam na
daktari wa Coastal Union ya Tanga, Dk. Mganaga Kitambi.
Pia
Herry ‘Mzozo’ Chibakasa wa Friends Rangers ya Dar es Salaam naye
atajadiliwa na Bunu Abdallah ambaye ni Kocha Msaidizi wa JKT Oljoro ya
Arusha.
Post a Comment