Busu la Penny lazua utata
Busu ambalo mtangazaji Peniel
Mungilwa ‘Penny’ amempiga mwigizaji Shamsa Ford limezua utata kufuatia
watu kumhusisha na tabia isiyofaa.
Hayo yalijiri hivi karibuni baada ya
mtangazaji huyo kutupia picha kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram
ndipo wafuasi wa mtandao huo walipoanza kumsema vibaya wakidai
anajiabisha kwa vitendo visivyofaa.
Alipoulizwa kuhusiana na jambo hilo,
Penny alisema: “Hayo ni maneno tu huwa hayani sumbui, lile ni busu la
kawaida. Nimembusu kama rafiki lakini nawashangaa hao wanaozua mambo yao
na kuzungumza tofauti.”
Post a Comment