Ruby, Maua Sama uso kwa uso na Ne-Yo, Mwanza
Staa wa R&B kutoka Marekani, Shaffer Smith ‘Ne-Yo’.
Na Andrew Carlos WAKALI wa sauti za kumtoa nyoka pangoni, Maua Saleh ‘Maua Sama’ pamoja na Hellen George ‘Ruby’ wanatarajiwa kukutana uso kwa uso na staa wa R&B kutoka Marekani, Shaffer Smith ‘Ne-Yo’, katika bonge la shoo litakalofanyika Mei 21, mwaka huu ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Akizungumza na Over Ze Weekend, mratibu wa shoo hiyo inayotambulika kama Jembeka Festival 2016, Sebastian Ndege alisema kuwa mbali na Maua na Ruby, usiku huo utakuwa pia maalum kwa mastaa kibao wakiongozwa na Diamond Platnumz.
Post a Comment