Mauno ya Snura yamdatisha staa wa muziki kutoka Nigeria, Don Jazzy
MAUNO ya mkali anayekimbiza kunako Muziki wa Mduara, Snura Mushi ‘Snura’ yameonekana kumdatisha staa wa muziki kutoka Nigeria, Don Jazzy kufikia hatua ya kuipongeza video ya bishosti huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Akichonga na Showbiz Xtra, Snura alisema
alipata taarifa juu ya Don kudatishwa na video hiyo iliyojaa mauno na
kwamba ni jibu kwa wanaoona muziki anaofanya hauendani na maadili.
“Kawaida ya Watanzania ni kusifia
visivyo vyao na kuponda vitu vya kwao. Sasa hilo ni tatizo maana wageni
wanakubali mambo tunayoyafanya. Mtu kama Don ambaye sina ukaribu naye
kusifia video yangu ni jambo kubwa,” alisema Snura.
Post a Comment