YANGA WAKABIDHIWA RASMI MZIGO WA WAARABU WA AL AHLY WA MISRI
Al
Ahly imeimaliza Libolo kwa mabao 2-0 katika mechi kali Waarabu hao
wababe wa soka wakiwa nyumbani. Sasa ni Yanga dhidi ya Ahly.
Yanga
imeitoa APR kwa mbinde kwa jumla ya mabao 3-2, sasa inakutana tena na
Al Ahly waliowatoa katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa.
Katika mechi ya leo, Al Ahly ilianza kupata bao lake katika dakika ya 10 Sobhy likadumu hadi mapumziko na kipindi cha pili ikafunga bao la pili kupitia Antui aliyemaliza kazi katika dakika ya 83.
Wakati
wanaitoa Yanga, Ahly walionekana kuwa wachovu, kwani walilazimika
kuwang’oa Yanga kwa mbinde wakiwa chini ya Kocha Hans van der Pluijm.
Pluijm
aliingoza Yanga kuitwanga Ahly bao 1-0 jijini Dar es Salaam,
iliposafiri hadi Alexandria, Yanga ikafungwa bao 1-0. Wakaingia kwenye
mikwaju ya penalti, ikang’oka.
Mbuyu Twite na Said Bahanuzi ndiyo waliopoteza penalti kwenye Uwanja wa Jeshi wa jijini Alexandria.

Post a Comment