WAKALA WA SHETANI - 01
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
WAKALA WA SHETANI
Kila mwanadamu yupo duniani kwa ajili ya kuishi, hakuna mwanadamu aliyeumbwa kupata mali kwa ajili ya kumpoteza mwenzake. Bali imeubwa riziki ya mtu ipitie kwa mtu. Wengi wamesahau kila kiumbe kitaonja mauti siku yake ikifika lakini si kwa utashi au tamaa za watu bali kwa mapenzi ya Mungu. Wengi huamini wataishi milele na kuwageuza wenzao kama chambo au ngazi ya kufikia utajiri au mafanikio kwa vile uhai wao unanukia harufu ya fedha. Ili kujua kwa nini uhai wa watu wengine una harufu ya fedha ungana tena na yuleyule mwandishi wako mahiri katika riwaya nyingine ya kusisimua Ally Mbetu…TUWE PAMOJA…
*******
Kilikuwa kiumbe cha ajabu ambacho japokuwa kilifanana na umbile la kibinaadamu lakini kilikuwa na matendo ya kinyama. Wengi walifikiri mzimu lakini haukuwa mzimu, alikuwa mwanadamu tena albino ambaye alionekana kuishi maisha marefu kama mnyama porini huku akiwa hana kiungo kimoja cha mwili cha mkono wa kulia.
Umbile lake lilikuwa lenye afya njema, nywele nyingi nyeupe na ndefu kama rasta. Ndevu nyingi kucha ndefu na mavazi yaliyochakaa yaliyoonyesha kutojua maji kwa kipindi kirefu zaidi ya mvua iliyomnyeshea.
Chakula chake kilikuwa nyama mbichi na matunda ya msituni. Macho yake yaliyokuwa mekundu na muda mwingi aliangalia chini. Alionekana kuwachukia wanadamu kuliko kitu chochote chini ya jua.
Siku ya kwanza kukutana naye naye aliua watu zaidi ya watatu, ilibidi itumike nguvu kwa kumpiga risasi ya kupoteza fahamu ndipo walipoweza kumkamata.
Daktari aliyepelekwa kwa ajili ya kumchunguza alinyongwa kwa kamba alizokuwa amefungwa nazo. Japo alikuwa kiumbe wa kawaida lakini mazingira yalimfanya aonekane yupo kama mnyama. Baada ya kumkata nywele na kucha bado alionekana mtu mwenye hasira asiyependa kutazama watu usoni.
Mkono mmoja uliokuwa umekatwa ulionyesha kovu la muda mrefu, lingekuwa bichi labda wangesema ni mmoja wa majeruhi wa kukatwa kiungo cha mkono katika janga lililolikumba taifa la kuuawa kwa kukatwa viungo walemavu wa ngozi albino.
Lakini alionekana mtu aliyeishi maisha ya porini kipindi kirefu japo haikufahamika ni muda gani alioishi sehemu ile. Pia jeraha la mkono aliokatwa lilionekana la muda mrefu sana.
Kingine ni hali ya kuwa kama mnyama asiyependa wanadamu zaidi ya kupenda wanyama. Tofauti yake nyingine, alikuwa na roho mbaya kuliko ya simba.
Hakupenda chakula kilichopikwa alipenda vyakula vibichi kama nyama mbichi na matunda, ndicho kilichokuwa chakula chake kikuu.
Waliitwa wataalamu wa kujua matatizo ya wanadamu walikutana na kumchunguza kwa muda. Vipimo vyote vilionyesha yupo katika hali ya kawaida. Umri wake ulionyesha ana miaka 35 na 40. Mmoja wa wataalamu aligundua kuwa mtu yule aliishi maisha ya porini kwa muda mrefu na hulka yake kuwa kama ya mnyama.
Walikubaliana kumtengenezea mazingira ya kumrudisha katika hali ya ubinaadamu. Pamoja na kuwa haongei lakini alionyesha kuna dalili za kusikia kilichozungumzwa kwani alikuwa makini kusikiliza kilichokuwa ikizungumzwa.
Mtaalamu waikolojia ya wanadamu aliwaeleza baada ya muda atarudi katika hali ya kawaida na kuamini mtu yule ana siri nzito ya kumfanya aishi maisha kama mnyama kwa muda mrefu porini na kuwa kiumbe mwenye hasira sana kisichopenda kutazama watu machoni.
Walimtengenezea mazingira ambayo yalikuwa yenye upendo huku muda wote akiwa peke yake huwekewa muziki wa taratibu wa vyombo vitupu. Mtaalamu waliwaambia kupitia muziki wa vyombo vitupu wa taratibu utajenga kifikra na kujiona ni mwanadamu huku wakimwekea picha za sinema zenye kuonyesha maisha ya upendo ya watu tofauti wakiwemo albino na watu.
***
Mtu yule aligunduliwa katika msitu mnene ulio pembezoni mji wa Mangu na wataalamu wa masuala ya utengenezaji wa mvua ambao waliletwa nchini kwa ajili ya kutengeneza mvua kutokana na taifa kukumbwa na janga la ukame lililosababisha mabwawa ya maji katika vyanzo vya umeme kukauka na kusababisha mgao wa umeme ulioliiingiza taifa kuyumba kiuchumi.
Marafiki wahisani wa nchi zilizoendelea walijitolea kuleta wataalamu wake kwa ajili ya kutengeneza mvua kwa bei nafuu. Nchi ya Thailand moja ya nchi marafiki walikubali kusaidia wataalamu pamoja na mitambo ili tuepukane na tatizo la ukame lililoikumba nchi yetu iliyokuwa na hatari ya kuingia gizani baada ya mabwawa yote kuwa kwenye hali mbaya kwa kina cha maji kupungua kila kukicha.
Kikosi cha wataalamu ambao kilizunguka sehemu yenye milima yenye miti mingi ambayo wangeweza kutengeneza mvua. Katika msitu wa Nyashana ulio pembezoni na mji wa Mangu waliuchagua na kuuona unafaa kuzalishia mvua pale.
Baada ya kuuchangua ile msitu walianza kazi mara moja kwa kuanza kupima. Wakiwa wanapima kwa kutumia kiona mbali waliweza kumuona mtu ambaye baada ya kumvuta karibu kwa mitambo ya kiona mbali walimuona kama mzimu na kuwashawishi kusogea karibu zaidi ili wamuone vizuri.
Walipomkaribia yule mtu ambaye wao walijua ni mzimu, alikimbia na kupotelea mapangoni. Walisitisha kazi ya kupima na kuanza kumtafuta yule mtu kutaka kujua mwisho wake na kwa nini yupo sehemu ile. Siku ya kwanza mpaka usiku unaingia hawakufanikiwa kumuona.
Wataalamu hawakukubali walipanga kurudi siku ya pili alfajiri na kujificha. Walifanikiwa kumuona majira ya saa moja asubuhi akitoka kwenye pango lake kwa kujinyoosha mwili.
Alipopiga miayo meno yake yalionekana yamedadilika rangi na kuwa kama ya simba weupe ilipotea kabisa. Mzungu mmoja alijitokeza mbele yake, yule mtu alipomuona alishtuka na kutimua mbio kwa kukwea miti na mawe kwa mkono mmoja kama sokwe.
Kila mmoja alipigwa na butwaa na kujiuliza kwa nini mtu yule yuko vile, suala ya mzimu walilifuta japo alikuwa na nywele nyingi ndefu makucha marefu na nguo chakavu.
Wapo waliodhani ni msukule baada ya kukimbia waliingia sehemu aliyotoka ndani ya pango lililokuwa na kiza kinene, kwa msaada ya tochi yenye mwanga mkali walifika hadi ndani ya pango. Ndani walikuta mifupa mingi ya wanyama matunda yaliyoliwa nusu nguo chakavu zilizokuwa kama godoro.
Hawakuishia hapa walizunguka kila kona lakini hawakukuta kitu kingine zaidi ya vile vitu walivyoviona. Kutokana na kuonekana mtu yule ni vigumu kumkataka walatengeneza mtego na kuondoka.
******
Siku ya pili walipofika walimkuta amenasa lakini akionekana kutaka kujinasua kwa kujitupa ovyo, walipomkaribia ili wamkamate aliwazidi nguvu kwa kutumia mkono mmoja aliweza kufanya uharibifu mkubwa kwa kuharibu vifaa ambavyo walivichukua kwa ajili ya kumrekodi mtu yule na kuua watu watatu.
Ilibidi wakimbie na kesho yake waende na bunduki yenye kutumia risasi ya kupunguza nguvu mwilini, apigwapo mtu huanguka lakini hafi. Ilibidi waende kwa taadhari kubwa wakiwa na baadhi ya wanajeshi wenye silaha kali kwa ajili ya kujihami.
Walifanikiwa kupiga risasi ya mgongo wakati akitaka kuwatoroka baada ya kuwashtukia. Alipopigwa alianguka chini na kupoteza fahamu, kufanikiwa kumchukua na kuondoka naye. Mtu yule baada ya kumuweka katika chumba ambacho wataalamu waliamini huenda atarudiwa na akili ili waweza kumuuliza vitu kama atakuwa na kumbukumbu navyo na sababu ya kuishi kule porini kama mnyama.
Baada ya kumuua daktari ilibidi wawe makini naye huku wakijitahidi kufanya uchunguzi zaidi kujua sababu ya kuishi maisha yake. Mwanzo muda wote alikuwa amechukia lakini kila siku zilivyokuwa zikienda ndivyo alivyokuwa akibadilika. Katika chumba walichomuweka walimwekea tivii ambayo walimwekea picha za katuni na za maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi waliokuwa wakiishi maisha ya upendo na watu tofauti.
Kuna siku wakati akiangalia katuni za Tom na Jerry aliangua kicheko mpaka machozi yakamtoka. Waliokuwa wakimfuatilia waliweza kugundua maendeleo makubwa kutokana na chombo kilichowekwa kurekodi matukio yake yote. Waliweza kumfungulia hata kukaa na watu bila kuonesha tabia za awali za kinyama na kuwachukia watu hata macho yake hakuangalia chini tena.
Taratibu aliweza kuwasiliana na watu kwa lugha ya Kiswahili cha kuungaunga chenye lafudhi ya Kisukuma. Baada ya kumrudisha kwenye afya yake, wana saikolojia walikaa naye kutaka kujua sababu ya yeye kuishi katika maisha yake. Baada ya kutulia kwa muda machozi yalianza kumtoka taratibu na kuweka michirizi juu ya mashavu yake kuonesha amekumbuka jambo lililouumiza moyo wake.
Baada ya muda mtaalamu aliyekuwa akimfuatilia toka mwanzo alimpa maji kwenye glasi na kumuomba ayanywe yote. Alikunywa maji yote na kutulia kwa muda kisha taratibu alianza kusimulia kisa kizima cha yeye kuishi porini kama mnyama kwa miaka yote hiyo bila kuonwa na mtu yeyote.
MIAKA 50 ILIYOPITA
Katika kijiji kimoja pembezoni mwa mji wa Mwanza karibu kabisa na ziwa Nyanza ambalo sasa hivi linaitwa Victoria. Majira ya saa mbili usiku Minza alikuwa akijigeuza katika kitanda cha kamba kilichotandikwa ngozi ya ng’ombe juu yale huku ameuma meno.
“Ngoshi wane…Mathayo.”( Mume wangu…Mathayo)
Alimwita mumewe kwa sauti ya chini huku akifinya shuka kwa vidole vya mkono wa kushoto na mkono mwingine kujipigapiga kwenye paja kutokana na maumivu ya uchungu wa kujifungua.
Mathayo aliyekuwa ametoka nje kuvuta gozo lake aliisikia sauti ya mkewe kwa mbali. Aliliweka gozo lake pembeni ya mlango na kuingia ndani ambako kibatari nacho kilikuwa kisisinzia kutokana na kuishiwa na mafuta.
“Mwana Bupilipili ginehe hange?” (vipi tena?)
“Nalebona makanza gashika.” (Muda umefika)
“Dogweta ginehe lolo?” (Tutafanya nini sasa?)
“Nene ango nalebyalela henaha do.” (Mimi najifungulia hapahapa.)
“Yayah nke wana doganhwitane o mama Sabina.” (Hapana mke wangu tukamwite mama Sabina.)
“Nale shaka hamo nagobyala mbelengw’elo bakomolaga” (Na wasiwasi wa kuzaa albino watamuua.)
“Ndoho odobyala mbelengw’elo hange.” (Hapana hatuwezi kuzaa tena albino.)
“Nalemaga nilekage nabyale ngw’enekele olo odohayaga no bebe jaga”( Nasema sitaki niache nizae mwenyewe kama hutaki na wewe ondoka.) Ngw’ana Bupilipili alikuwa mkali baada ya kuona mumewe hamuelewi.
Mathayo hakuwa na jinsi alikubaliana na mkewe kumzalisha mwenyewe. Sababu kubwa ya mkewe kukataa kumwita jirani yao mama Sabina ili aje amzalishe ilitokana na desturi ya pale kijijini unapojifungua mtoto albino hutengwa kwa kufukuzwa kijiji alichopo au mtoto wako kuuawa kwa kupewa sumu.
Miaka miaka miwili iliyopita ngw’ana Bupilipili alijifungua mtoto wa kike ambaye alikuwa albino uongozi wa kijiji uliwaeleza wachague kitu kimoja kufukuzwa kijijini au mtoto auawe. Ngw’ana Bupilipili alikubali kufukuzwa lakini mumewe alikubali mtoto auawe.
Ilikuwa vita kubwa kati ya mume na mke baada ya mtoto wao kuuawa, ilibidi familia ya mke na mume kuingilia kati ikiwa pamoja na tambiko ili tatizo lile usitokee tena kwenye familia. Wao waliona ni mkosi mkubwa mtu kuzaaa mtoto albino.
Hali ile iliendelea kila siku kwa familia zote zilizozaa mtoto albino pale kijijini watoto wao kuuawa kwa kuonekana mikosi au kufukuzwa kijijini kama wakigoma mtoto wao kuuawa.
Wakiondoka na kwenda porini walitumwa vijana waliokwenda kumpora yule mtoto na kumuua. Wanawake wote kijijini walikuwa katika hali ya wasiwasi kwa kila mwanamke aliyebeba ujauzito alikuwa katika wakati mgumu mpaka atakapojifungua na kukuta mtoto wa kawaida.
Ngw’ana Bupilipili toka abebe ujauzito amekuwa hana raha kwa kumuomba Mungu usiku na mchana asizae tena mtoto albino hata kupanga siku ya kujifungua iwe siri kati yake na mumewe tu. Kila siku alimuomba Mungu asizae mtoto albino aliogopa kumpoteza tena japokuwa moyoni alijiapiza hata kuwa tayari mwanaye auawe na kuwa tayari kutengwa na kijiji na atakaye muua lazima kwanza amuue yeye.
Ilibidi adanganye kwa kurudisha siku za ujauzito wake nyuma, kila alipoulizwa kuhusu ujauzito wake una miezi mingapi. Alirudisha miezi miwili nyuma ili atakapo jifungua ajue afanye kitu gani kama atajifungua mtoto albino.
Ndipo siku ya kujifungua ilipowadia hakutaka aitwe mtu yeyote kushuhudia anazaliwa mtoto gani kwa kuhofia siri yake kutoka nje kama atajifungua mtoto albino. Mumewe baada ya kukatazwa na mkewe asimwite mtu yeyoye aliamua kumsaidia mkewe kujifungua.
Kwa vile alikuwa na uzoefu aliweza kumsaidia mkewe kujifungua mtoto salama. Baada ya huduma zote mtoto alilazwa pembeni huku wakijitahidi kuzuia sauti ya mtoto kabla ya kujua mtoto aliyezaliwa ni wa aina gani ni albino au wa kawaida.
Mathayo baada ya kumhudumia mtoto wake na mkewe ambaye aliweza kukaa mwenyewe, kazi akawa kumtazama mtoto aliyezaliwa wa aina gani. Uchunguzi ulionesha mtoto yule ni albino. Walijikuta wote wakikosa raha hasa ngw’ana Bupilipili ambaye aliamini ana mtihani mkubwa wa kumpoteza tena mtoto mwingine ambaye amekaa naye tumboni kwa kipindi kirefu halafu watu wamchukue na kwenda kumuua kiurahisi.
Itaendelea kesho

Post a Comment