UBISHI WA MESSI, RONALDO WASABABISHA SHABIKI KUMUUA RAFIKI YAKE INDIA, WOTE NI WANATOKEA BARANI AFRIKA
Suala
la ushindani wa washambuliaji Lionel Messi dhidi ya Cristiano Ronaldo
sass limekwenda mbali baada ya rafiki kumuua mwenzake nchini India.
Michael
Chukwuma, 21, anashikiliwa kwa mauaji ya rafiki yake Obina Durumchukwu
mwenye umri wa miaka 34, aliyeuwawa kwa kuchomwa na kipande cha glasi
baada ya ubishi huo katika jimbo dogo ala Nallasopara jijini Mumbai,
jana Jumapili.
Inspekta
wa Polisi wa jijini la Mumbai, Kiran Kabadi amethibitisha kushikiliwa
kwa Chukwuma ambaye alimuua mwenzake baada ya kupigwa usoni na glasi
ambayo ilivunjika.
“Ni
marafiki wawili, siku moja kabla walisherehea sikukuu ya kuzaliwa ya
Chukwuma. Asubuhi yake wakaamkia katika mpira, ubishi uliwafikisha
pabaya.
“Mmoja
aliamini Messi ni bora na mwingine akasema Ronaldo. Walipoona
wameshindwa kuelewana, Durumchukwu alirusha glasi iliyompata Chukwuma
usoni na kusababisha majeraha kidogo.
“Kutokana
na hasira, Chukwuma naye aliichukua sehemu ya vipande vya glasi ile na
kwenda kumchoma navyo rafiki yake hadi alipopoteza maisha,” alisema.
Messi
na Ronaldo ndiyo wachezaji wenye upinzani mkubwa duniani kote huku kila
mmoja akiwa na mashabiki wanaoamini wanayemuunga mkono ni bora zaidi.
Hapa nyumbani Tanzania, ubishi huo umekuwa ni jambo la kawaida kutokea na wakati mwingine pia kusababisha hasira.

Post a Comment