MURO ATAMBA SIMBA WAPO KILELENI WANATALII, YANGA ITAREJEA TENA
Yanga
wamejigamba wao ndiyo watu wa ‘kileleni’, akiamini wapinzani wao Simba
wanatalii tu kwani Yanga watarejea kwa kushinda mechi yao kesho.
Kesho Yanga itakuwa mwenyeji wa African Sports kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Msemaji
na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro
amesema Yanga itaindika African Sports na kurejea kileleni.
Muro anaamini Simba ambao wako kileleni kwa sasa wamekaa kwa muda tu.
“Wamekaa
kwa muda tu zetu, hata wao wanajua ile si nafasi yao. Kesho
tutawatandika African Sports, tunaomba Mungu atusaidia tufunge mabao
mengi zaidi,” alisema.
Simba
ina pointi 48 ikiwa kileleni mwa Ligi Kuu Bara, Yanga na Azam FC
wanafukuzana katika nafasi ya pili kila mmoja akiwa na pointi 47.
Lakini
Yanga na Azam FC kila upande una mchezo mmoja mkononi na kama
zitashinda zote, Simba itaporomoka tena hadi katika nafasi ya tatu.

Post a Comment