MASHABIKI RAYON WATUA KWENYE MAZOEZI YA YANGA, BASI NI FULL NYIMBO MWANZO MWISHO

Yanga ipo Kigali, Rwanda kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya APR. Itapigwa kwenye Uwanja wa Amahoro, kesho.
Pamoja
na kuwa ugenini, Yanga wala haina shida ya mashabiki kwa kuwa tayari
mashabiki wa Rayon Sports wameishajitokeza kuiunga mkono kwa nguvu.
Katika mazoezi yake kwenye Uwanja wa Ferwafa eneo la Remara jijini Kigali, mashabiki wa Rayon Sports ambao ni wapinzani wakubwa wa APR walijitokeza mazoezini na kuiunga mkono Yanga kwa nyimbo na machombezo.
Hali ambayo inaonyesha, kesho watakuwa uwanjani kuendelea kuiunga mkono kwa nguvu zote.
APR
na Rayon zina upinzani mkubwa katika soka nchini Rwanda kama ilivyo kwa
Yanga na Simba nchini Tanzania. Hivyo mashabiki wa Rayon wanataka kuona
APR ikiadhibiwa na Yanga hiyo kesho.
Post a Comment