Gigy Money: Bila shilingi milioni 1 humpati kwenye video yako
Gift Stanford ‘Gigy Money’.
MUUZA nyago kwenye
video mbalimbali za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kwa mara ya
kwanza amefungukia ishu yake ya malipo kupitia video za Bongo Fleva
anazofanya kama ‘Video Queen’ kuwa kwa sasa bila shilingi milioni moja
humpati.
Akichonga na Showbiz
Gigy alisema kuwa, kwa sasa Muziki wa Bongo Fleva umebadilika na hata
video zake zina viwango vikubwa tofauti na kipindi cha nyuma ambapo hata
makampuni ya video yalikuwa machache hivyo kwa wale mastaa yupo tayari
kuwafanyia kuanzia laki tano lakini kwa wale ambao hawana majina sana
‘chipukizi’ bila milioni moja hawampati.
“Kwa kawaida video nyingi huwa naanzia
laki tano lakini kuna video ambazo kiukweli kabisa bila milioni moja
siwezi kufanya,” alisema Gigy.
Gigy ametokelezea kwenye video kibao za
Bongo Fleva ambazo ni Siachani Nawe ya Barakah Da Prince, Get High ya
Godzilla, Shika Adabu Yako ya Nay wa Mitego na nyingine nyingi.
Post a Comment