ad

ad

Breaking News: Bulaya akamatwa na Polisi jijini Mwanza



 
 Mbunge  wa Jimbo la Bunda Chadema, Esther Bulaya.

Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene  leo  amesema mbunge  wa Jimbo la Bunda Chadema, Esther Bulaya, amekamatwa na polisi Mwanza, leo usiku hotelini, sababu za kukamatwa hazijulikani.


Polisi walivamia Hoteli aliyofikia mbunge huyo na kumkamata majira ya saa 7 usiku na kisha  kumpeleka  kituo cha kati cha Jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mhe. Halima Mdee (Mb) , Joyce Sokombe (Mb) pamoja na Wakili John Malya.
 

Hadi sasa anashikiliwa na polisi. Viongozi wa Chadema  wanaelekea kituo cha polisi muda huu kujua hatma yake.

No comments

Powered by Blogger.