AL AHLY KUTUMIA MECHI YA APR KUIMALIZA YANGA, KOCHA WAO AANZA KAZI
![]() |
| APR |
Baada ya kupata mkikanda mitatu ya Yanga, Al Ahly imeanza kuifanyia kazi kupitia kocha wake, Martin Jol raia wa Uholanzi.
Lakini
taarifa zinaeleza, mechi ya kwanza ambayo kocha huyo ameanza kuifanyia
kazi ni ile Yanga iliyocheza mjini Kigali na kuifunga APR ya Rwanda kwa
mabao 2-1.
| YANGA |
Kwa
mujibu wa Mtanzania anateishi nchini Misri anaamini kocha huyo, lazima
ataanza na mkanda huo kuiona Yanga inaposhiriki michyano ya kimataifa.
“Unajua
wamepata mikanda mitatu, nimeambiwa mechi mbili ni Yanga akicheza mechi
za Ligi Kuu Tanzania. Nafikiri kwa Jol lazima atataka wakati Yanga
ikicheza mechi za kimataifa.
“Mechi
dhidi ya APR inaweza ikawa msaada mkubwa kwa kocha huyo kwa kuwa
atataka kuwajua Yanga wanachezaje wakiwa nje ya Tanzania na hasa katika
michuano ya kimataifa,” alisema.
“Najua
mfumo wao, kocha atasoma kila kitu halafu watakaa pamoja na kuchambua
huku wakichangia nini cha kufanya,” alisisitiza Mtanzania huyo anayeishi
nchini Misri kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Al Ahly itakuwa ya kwanza kusafiri ugenini, itaivaa Yanga Aprili 9 kabla ya mechi ya marudiano.

Post a Comment