Wolper, Mkongo watimkia Sauzi!

DAR ES SALAAM:
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper na mpenzi wake Mkongo,
wamedaiwa kuuza magari yao na kutimkia nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya
jina, kimepenyeza ubuyu kuwa miezi kadhaa iliyopita, maisha ya Wolper na
Mkongo huyo yalibadilika na kuwa magumu hivyo katika kusaka suluhisho
la kujikwamua, wakaamua kuuza magari yao na kwenda kuanzisha maisha
mapya Sauz.
“Jamani mambo hapa kati hayakuwaendea
vizuri Wolper na mpenzi wake hivyo waliamua kutimkia Sauz lakini waliuza
magari yao na kwenda kuendelea na maisha mengine huko maana Mkongo
alikuwa pia na makazi kule,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuinyaka habari hiyo gazeti
hili liliwasiliana na Wolper kwa njia ya simu ambapo alikiri kuwa yupo
Sauz na mpenzi wake Mkongo lakini akakana vikali suala la wao kuuza
magari.
“Jamani kwa nini watu wako hivyo mimi
sijauza gari langu lolote kama huamini nenda nyumbani utayakuta watu
wanapenda sana kuzungumza vitu ambavyo hawana uhakika navyo kabisa.
“Tuliamua tu na mpenzi wangu tubadili maisha, tuhamie huku Sauz na si kwamba maisha Bongo yalikuwa magumu,” alisema Wolper.
Post a Comment