Uwanja wa Kaitaba waifilisi Kagera Sugar
Dar es Salaam
UONGOZI wa Kagera Sugar umeibuka na kutoa tathmini ya madhara waliyoyapata juu ya ukarabati wa Uwanja wa Kaitaba ambao huutumia kama uwanja wa nyumbani ambao umekuwa kwenye matengenezo kwa msimu wa pili sasa.
Kutokana na matengenezo hayo, Kagera inaishi kwa kukodi viwanja kucheza mechi zake za nyumbani huku misimu yote timu ikiishi na kula hotelini, gharama ambazo wanasema isingekuwa timu ya kiwanda pengine wangekuwa wameshanyoosha mikono kutokana na ukubwa wa bajeti.
Mratibu wa kikosi hicho, Mohammed Hussein amesema:
“Hela za wadhamini wa ligi kuu kwetu hazina maana. Kitendo cha kuweka kambini wachezaji 28 hotelini kila siku kula na kulala ni gharama kwa misimu miwili, ni timu gani inaweza kuhimili hili.
Timu hiyo ilianza kukodi Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ikahamia Kambarage, Shinyanga kisha Alli Hassan Mwinyi wa Tabora na sasa imerejea Kambarage.

Post a Comment