Linah alala na Wizkid hotelini
Stori: Musa Mateja, Wikienda
Dar es Salaam: Imefichuka! Hatimaye ishu ya wanamuziki
wa Bongo, Estelina Sanga ‘Linah’, kudaiwa kulala kitanda kimoja na msanii wa
muziki kutoka Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’, imebumburuka.
Baada ya kuandamwa na skendo hiyo ya kutoka kimapenzi na
Wizkid huku mashabiki wake waliyo wengi wakishindwa kuamini juu ya uhusiano
huo, hatimaye sasa mambo yamevuja na kujidhihirisha kuwa kweli staa huyo alilala
hotelini tena kitanda kimoja na Mnigeria huyo.
Kikieleza kwa kujiamini, kiliweka wazi kuwa Linah
alilala kitanda kimoja na staa huyo kwenye hoteli moja iliyopo Masaki, Dar, baada
ya msanii huyo kutua Bongo kwa ajili ya kufanya makamuzi kwenye moja ya shoo
zake alizokuwa ameletwa na promota King Solomon.
“Linah alilala na Wizkid, alikaa naye hadi siku
anaondoka kulelekea Nigeria, na nikwambie ukweli uliyojificha ni kwamba, Linah
kumbe ni siku kibao alikuwa akiwasilina na Wizkid kupitia mtandao wa Insta
Direct, lakini hawakuwahi kuonana ila nafasi ya kuonana na kulala pamoja
ilikamilika baada ya Wizkid kuja Bongo,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kumwagiwa ishu hiyo, gazeti hili ‘lilicheki’ na
Linah ambaye alikiri ‘kubanjuka’ na Wizkid huku akidai kwamba kuna mtu alifuta
kila kitu kwenye simu yake hasa kilichohusiana na Wizkid wakati yeye alikuwa na
mipango mingi naye.
Alisema kitendo alichofanyiwa na mtu huyo ambaye aliwahi
kuwa mpenzi wake kimemhuzunisha mno kwani ndoto zake za kufanya ngoma na staa
huyo zimeyeyuka.




Post a Comment