Breaking News: Rapper John Woka afariki dunia leo jijini Dar
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Michael Dennis Mhina 'Joni Woka'.
Akiongea
kwa simu kaka wa marehemu Omari Milay, amesema walipigiwa simu alfajiri
ya leo na kujulishwa kuwa Joni Woka amefariki katika hospitali ya
Muhimbili, alipokuwa akipata matibabu ya ajali aliyopata siku ya jana.
Joni
Woka alipata ajali ya kugongwa na kitu kizito kwenye paji la uso,
alipokuwa garage maeneo ya Sinza akitengeneza gari yake, kwa bahati
mbaya mtungi wa gesi ukalipuka na moja ya vipande vya chuma chenye ncha
kali kikamchoma kichwani,
Tarifa za awali za madaktari zilisema wanahofia kipande hiko kimefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.
Mipango ya mazishi familia imesema inakutana kujadili na mara itakapokamilika watajulisha watu nini kinaendelea.
Msanii John Woka ambaye alikuwa kwenye kundi la Watukutu Family, alijipatia umaarufu kwa nyimbo zake za Sophia, baby gal na nyinginezo, ambazo aliziimba kwa mtindo wa ulevi.
Kwa yeyote aliyeguswa na angependa kutoa rambi rambi anaweza kuwasiliana na kaka yake kwa namba +255767007005.

Post a Comment