KOMBE LA MAPINDUZI LAGOMA KUBAKI TANZANIA, WATOTO WA MUSEVENI WAONDOKA NALO KWAO
Wachezaji wa URA FC wakishangilia ubingwa wao
Unaweza ukasema kisicho riziki hakiliki, hiyo ni baada ya timu ya
Mtibwa Sugar kulikosa tena kombe la Mapinduzi Cup kwa mwaka 2016
kufuatia kupoteza mchezo wa fainali kwa magoli 3-1 dhidi ya URA ya
Uganda kwenye mchezo uliochezwa usiku wa Jumatano January 14, 2016
kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.URA walianza kupata bao la kwanza dakika ya 16 kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Julius Ntambi bao ambalo lilidumu kwa dakika zote 45 za kipindi cha kwanza.
Peter Lwasa aliyetokea benchi ndiye aliyezima ndoto za Mtibwa kuibuka mashujaa wa kombe la mapinduzi mwaka huu baada ya kutupia bao mbili kambani na kuihakikishia timu yake ushindi na kubeba ndoo ya Mapinduzi. Lwasa alipachika wavuni magoli yake dakika ya 85 na 88 kipindi cha pili.
Mshindi wa Mapinduzi Cup ametwaa kitita cha shilingi milioni kumi taslimu wakati mshindi wa pili amejinyakulia shilingi milioni tano.
Kesho Mtibwa watarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mwendelezo wa mechi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambapo Jumamosi watakutana na Simba SC ambao waliwatupa nje ya mashindano ya Mapinduzi kwenye hatua ya nusu fainali.

Post a Comment