Kajala gonjwa gonjwa...kisa kusumbuliwa na ujauzito
Kajala gonjwa gonjwa
Staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja amekuwa mgonjwa mgonjwa anayekwenda hospitalini mara kwa mara huku kukiwa na madai kuwa hali hiyo inatokana na kusumbuliwa na ujauzito alioripotiwa kuwa nao hivi karibuni.
Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo, kilisema Kajala amekuwa akiugua mara kwa mara jambo ambalo pia linampa shida ya vyakula kwani kila anachokula anajikuta akirudisha ‘chenji’ (kutapika).
“Yaani Kajala anateseka sana, amekuwa akiumwaumwa tu pia vyakula vyake ni vya kuchagua sana kwani mara nyingi akila tu anatapika, lazima kuna kitu,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Kajala ambaye alijibu kwa kifupi;
“Ni kweli nimekuwa nikiumwaumwa kila wakati ila namwachia Mungu ndiyo anajua kila kitu.”Kajala ni mama wa mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Paula.

Post a Comment