Genevieve anunua nyumba za kifahari za milioni 300
Mkongwe kunako filamu Nollywood, Genevieve Nnaji.
MKONGWE kunako filamu Nollywood, Genevieve Nnaji hivi karibuni
alifanikiwa kununua nyumba za kifahari zenye thamani ya Naira milioni 39
(zaidi ya milioni 300 za Kitanzania) zilizopo pande za Apo Dutse,
Abuja.Mbali na kununua nyumba hizo, kupitia ukurasa wake wa Instagram, staa huyo mwenye kubamba katika filamu za majonzi, aliposti picha za majengo hayo ambayo yalikuwa bado katika ukarabati lakini aliambulia ‘za chembe’ kutoka kwa mashabiki wake.
Moja ya komenti za mashabiki wake, ilimtaka aachane na kile kinachosemekana ni upuuzi na ulimbukeni wa kujenga eneo ambalo si walipotokea.
Kila siku utasikia wapo Dubai, Afrika Kusini, Ulaya, Marekani na kuweka maendeleo yao huko,” ilisomeka moja ya koment ya mashabiki.
(Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL)

Post a Comment