ad

ad

Dar waendelea kuchangamkia bahati nasibu ya Shinda Nyumba


 ZIKIWA zimepita siku chache baada ya Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, mapema leo wakazi wa maeneo ya Tandale, Kigogo na Magomeni jijini Dar es Salaam, wameonekana kuchangamkia kununua magazeti ya Global Publishers ili kuweza kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd.
Katika bahati nasibu hiyo, msomaji anatakiwa kununua magazeti na kukata kuponi, kisha kuijaza na kuituma kwa njia ya posta au kuifikisha moja kwa moja katika ofisi za Global, Bamaga, Mwenge, Dar au hata kuwafikishia kwa mawakala wa kuuza magazeti waliopo hapa nchini.
Droo ya kwanza ya bahati nasibu hiyo inatarajia kuchezeshwa Januari 7, mwaka huu katika viwanja vya Mbagala Zakhem, Dar huku zawadi mbalimbali kama simu za kisasa, dinner sets (vyombo vya ndani, bed sheets, TV, Ving’amuzi vya TING na Pikipiki vitatolewa kwa washindi.
Wafanyakazi wa Global, ndugu zao na watu walio chini ya umri wa miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki.









Powered by Blogger.