Arusha; Denti aliyedai kubakwa na polisi hofu yatanda
ARUSHA: HOFU! Simulizi ya mwanafunzi wa Sekondari ya Wasichana Korogwe kudai alibakwa na kujeruhiwa na askari polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Arusha, aliyemtaja kwa jina moja la Rafael bado inauma miongoni mwa wakazi wa jiji hili, Amani linachambua. Baadhi ya wakazi wa Jiji la Arusha, juzi walimiminika kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru ili kumjulia hali mwanafunzi huyo na kumpa pole.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kama madai ya denti huyo ni ya kweli, watu watapoteza imani na jeshi hilo na kuwazidishia hofu. Akizungumza kwa uchungu akiwa wodi ya majeruhi katika hospitali hiyo, mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) alisema alikumbwa na mkasa huo saa 2 usiku wa Januari 16, mwaka huu eneo la Kwamorombo wakati akienda kwa ndugu yake anayeishi eneo hilo akitokea Mwanza. “Nilitoka Mwanza, nikashuka Arusha. Nikakata tiketi ili kesho yake niende Korogwe shuleni. Hivyo ilinibidi nikalale kwa ndugu yangu.
“Nikiwa njiani, nilihisi kupotea, nikamuomba msaada kijana mmoja anipe simu niwasiliane na huyo ndugu yangu. “Nikiwa nataka kuongea ghafla alitokea polisi akiwa amevaa sare na kumuambia yule kijana aniache, aondoke. “Yule askari akanitolea kitambulisho chake cha kazi, akaniambia nipo kwenye mikono salama, akaniambia nimfuate anipeleke Kituo cha Polisi cha Mbauda kwa msaada zaidi wa ninakokwenda,” alisema denti huyo.
Alisema, baada ya umbali mrefu askari huyo akawa anaelekea porini hali iliyompa wasiwasi na kumuuliza, akajibiwa wanakaribia kufika. “Ghafla alinipiga ngwara kisha akaniambia pale ndiyo kituo cha polisi. Nilipiga kelele kuomba msaada, sikufanikiwa. Akanipiga teke la mdomoni, akaninyonga halafu akanipiga mateke mgongoni na kuniamuru nivue nguo.
“Baada ya kukataa alinivua kwa nguvu kisha akaanza kunibaka mpaka nikapoteza fahamu. Nilizinduka saa tisa usiku, nikamwona akipekua begi langu, akachukua shilingi 170,000 za karo ya shule na za maandalizi ya
mahafali yatakayofanyika Aprili mwaka huu.
“Baada ya kuona nimezinduka anililazimisha nimnyonye sehemu zake za siri, ndipo nilipofanikiwa kumng’ata akanipiga tena na kutoweka,” alisema. Alisema alijikokota kwa shida mpaka kituo cha mafuta, akaomba msaada ambapo wafanyakazi wa hapo walimpeleka Kituo Kikuu cha Polisi Arusha ambapo aliandika maelezo na kupelekwa hospitali kwa matibabu. Mwanafunzi huyo alipelekwa tena polisi na kuambiwa anatakiwa kumtambua askari aliyedai kumbaka ambapo gwaride la utambuzi lilifanyika na kumwona japo askari huyo alibisha.
“Alipobisha niliwaambia wamwangalie sehemu za siri nilimng’ata, wakakuta ni kweli. Nimeumizwa sana, nimekatizwa masomo. Muda huu ningekuwa shuleni,” alisema. Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Jacqueline Urioh alikiri kumpokea mwanafunzi huyo akiwa katika hali mbaya. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas alisema kwa sasa hawezi kuzungumza na vyombo vya habari juu ya tukio hilo na kuahidi kufanya hivyo baada ya upelelezi kukamilika.
CHANZO: GPL

Post a Comment