Airtel yazindua Duka la kisasa jijini Dar es Saalam
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi,
na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani akiongea wakati wa uzinduzi wa duka
jipya la kisasa la Airtel Expo lililopo katika makao makuu ya Airtel
Morocco, jijini Dar es Saalam. Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn
Sunil Colaso akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasilino wa Airtel Bi.
Beatrice Singano Mallya.
Afisa huduma kwa wateja wa
Airtel, Deogratius Gerald (kulia) akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng. Edwin Ngonyani juu ya huduma
zinazopatikana katika duka jipya wakati wa uzinduzi wa duka
hilo. Wakishuhudia (kutoka kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mawasiliano, Prof. Faustine Kamuzora, Naibu Katibu Mkuu Dr Mary Sasabo
na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw. Sunil Colaso.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi,
na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani akiongea na waandishi wa habari
wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Airtel Expo lililopo
katika makao makuu ya Airtel Morocco,jijini Dar es Saalam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi,
na Mawailiano Eng. Edwin Ngonyani pamoja na mkurugenzi mkuu wa Airtel
kwa pamoja wakibonyesha kitufe kuashiria uzinduzi wa duka la Airtel Expo
lililopo makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
Shamrashamra za uzinduzi wa duka la Airtel Expo Morocco, jijini Dar es Saalam
Afisa huduma kwa wateja wa
Airtel, Deogratius Gerald,(kwanza kushoto) akimuonyesha Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani vifaa na simu
mbalimbali vinavyopatikana katika duka jipya la Airtel Expo wakati wa
uzinduzi rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel
Morocco, jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel
Bw. Sunil Colaso (wa kwanza kulia) akifatiwa na Meneja huduma kwa wateja
bi, Zakia Omary.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi,
na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani akimsikiliza Mkurugenzi wa huduma kwa
wateja wa Airtel, Bi Adriana Lyamba na meneja huduma kwa wateja Zakia
Omary (katikati) wakati wa uzinduzi rasmi wa duka hilo jana katika ofisi
za makao makuu ya Airtel Morocco, jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso.

Post a Comment