Ubunge wa Saed Kubenea Wapingwa Mahakamani

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.
Aliyekuwa
mgombea ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.
Didas Massaburi, amefungua kesi ya kupinga ushindi wa Saed Kubenea,
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Dk. Massaburi amefungua kesi hiyo ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Mbali
ya Kubenea, wengine waliounganishwa katika kesi hiyo ni Masimamizi wa
Uchaguzi katika jimbo hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Katika
kesi hiyo, Dk. Massaburi anadai kwamba mshtakiwa wa kwanza (Kubenea),
alitoa rushwa ya kununua jenereta katika hospitali ya Mavurunza iliyopo
kata ya Kimara, kutoa rushwa ya ujenzi wa barabara ya Matete, kutoa
zawadi kwa kununulia ‘Pool Table’, kwa ajili ya kuwashawishi wananchi
wampigie kura.
Madai dhidi ya Msimamizi wa
Uchaguzi wa jimbo hilo ni hakumpatia nafasi ya kuhesabu kura upya kama
alivyoomba, hakumjulisha tarehe, muda na wapi matokeo ya jimbo hilo
yalikuwa yanajumulishwa, yeye na mawakala wake hawakuona wakati vifaa
vya uchaguzi vinafunguliwa.
Pia anadai kwamba
baadhi ya vituo havikufanya uchaguzi, na pia baadhi ya wapigakura
walipiga kura wakati hawajafikisha umri wa kupiga kura.
Katika madai hayo, Dk. Massaburi anaiomba Mahakama Kuu itengue ushindi wa Kubenea uliotangazwa na Msimamzi wa Jimbo hilo.
Post a Comment