ad

ad

Shilole angusha pati ya kufunga mwaka

 STAA anayewakilisha kwenye tasnia ya filamu na Bongo Fleva, Zuwena Mohame 'Shilole', usiku wa kuamkia leo ameangusha bonge la pati la nyumbani  kwake Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ambapo aliteketeza kiasi cha sh.  mil. 3, kwa kununua mbuzi wanne na kuku zaidi ya 50, huku vinywaji vya kila aina vikitawala pati hiyo kiasi cha kuwafanya waalikwa kunywa hadi kusaza.

Akizungumzia maandalizi hayo Shilole alisema kwamba, pati hiyo ina maana ya kujipongeza kutokana na misukosuko mbalimbali aliyoipata kwa muda wa mwaka mzima, mbali na hivyo, Shilole alisema kwamba, ameamua kuandaa vitu vyote ili apate muda wa kubadilishana mawazo na baadhi ya wasanii na marafiki zake ambao amekuwa akishirikiana nao kwa mambo mengi katika harakati zake za kusaka mkate wa kila siku.

"Nimeamua kuandaa pati hii kwa lengo la kutaka kukaa na wasanii na marafiki zangu ili tuweze kubadilishana mawazo, lakini mbali na hivyo pia nimeamua kusherehekea kutokana kwamba tunaelekea kwenda kufunga mwaka ambapo nimepitia mihangaiko mikubwa kwenye familia yangu na leo naona kama mambo yanaanza kunyooka baada ya mambo fulanifulani kuachana nayo," alisema Shilole.









Powered by Blogger.