Wastara kukatwa mguu tena! Ashindwa kulala kwa maumivu..
Imelda Mtema
MASKINI wa Mungu!
Baada ya kupata faraja kwa miaka kadhaa kwa kuwekewa mguu wa bandia,
mwigizaji wa sinema za Kibongo, Wastara Juma, amepatwa na masaibu
mengine ya kutakiwa kukatwa tena sehemu ya mguu uliokuwa umewekewa mguu
wa bandia, Risasi Jumamosi lina stori nzima ya kusikitisha.
TATIZO LILIPOANZIA
![]() |
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu
na Wastara ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, tatizo
linalosababisha mwigizaji kutakiwa kukatwa mguu huo wa kushoto
lilimuanza alipokuwa kwenye kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM)
zilizomalizika Oktoba 24, mwaka huu.

“Tatizo
lilimuanzia akiwa kwenye kampeni za CCM. Nafikiri kwenye mishemishe
zile za kupanda majukwaani aliushtua, sasa ukawa unamuuma na yeye
hakuweza kubaini mara moja tatizo ni nini. Kumbe mguu wake wa bandia pia
ulikuwa umekatika vidole na kulika kwa chini ya unyayo.
ATESEKA USIKU
“Alikuwa
hapati usingizi usiku, ilibidi awe anakunywa dawa za kutuliza maumivu
kila siku ndiyo aendelee na safari za kampeni kesho yake,” alisema ndugu
huyo wa karibu wa Wastara.
AWASAKA MADAKTARI WAKE
Ndugu huyo alizidi kueleza kuwa, baada
ya Wastara kumaliza kampeni, aliwasiliana na madaktari wake waliomtibu
awali nchini Kenya ambao walimshauri awatumie picha ya eneo alilokuwa
akisikia maumivu pamoja na mguu mzima wa baindia.
Madaktari
hao baada ya kubaini mguu huo wa bandia umechoka na kusababisha tatizo
la uvimbe, walimwambia anahitajika kukatwa sehemu ya mguu wake na
kuwekewa mguu mwingine wa bandia.
“Aliwatafuta
madaktari wake Kenya, wakamwambia hakuna ujanja kwa sehemu hiyo ilikuwa
imevimba inatakiwa kukatwa ili aweze kuwekewa mguu mwingine,” alisema
ndugu huyo.
WASTARA MWENYEWE
Baada
ya kuzungumza na ndugu huyo, mwanahabari wetu alimtafuta Wastara
mwenyewe ambaye alieleza kwa kirefu kuhusiana na tatizo hilo.
“Unajua
nilipokuwa kwenye kampeni, nilianza kusikia maumivu makali mno,
nafikiri ni kutokana na kule kukimbiakimbia hivyo ilikuwa lazima ninywe
dawa ya kupunguza maumivu kila wakati.
“Niliporudi
ilibidi niombe ushauri kwa madaktari wangu ambao walinishauri
niuchunguze vizuri mguu na niwatumie picha wao, nilipofanya hivyo
niligundua mguu wangu wa bandia umekatika vidole viwili pia kwenye nyayo
umeharibika sana,” alisema Wastara.
Mwigizaji
huyo aliendelea kueleza kuwa tatizo hilo la kukatika vidole na nyayo
kuharibika ndilo lililosababisha apate uvimbe ambao baadaye ulimfanya
ashauriwe kukatwa kidogo ili kuwekewa mguu mpya wa bandia.
MILIONI TATU ZAHITAJIKA
“Hapa
ninapokuambia mimi natakiwa milioni tatu kwa ajili ya kuweka mguu
mwingine na nina maumivu makali sana yasiyopungua kila siku mpaka
najiuliza hatma yangu jamani naumia.
“Nipo
katika mawazo sana, nikifikiria kukatwa tena mguu wangu yaani ni mateso
juu ya mateso Mungu anisaidie kwa kweli maana mitihani hii kila siku
mimi jamani,” alisema Wastara.
TUJIKUMBUSHE
Machi
12, 2009 wakati huo wakiwa wachumba tu, Wastara na marehemu Sajuki
Juma, walipata ajali mbaya ya pikipiki maeneo ya karibu na walipokuwa
wanaishi, Tabata, Dar es Salaam ambapo mwanadada huyo alivunjika mguu na
kuharibika vibaya.
Baada
ya hapo, Wastara alilazimika kukatwa mguu nchini Kenya na kuwekewa wa
bandia kisha baadaye akafunga ndoa na marehemu mumewe, Sajuki.
CHANZO: RISASI JUMAMOSI


Post a Comment