Wastara ampa ampa kichapo bondi
Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma
Brighton Masalu
KAZI ipo!
Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma anadaiwa kumpa kichapo kikali
aliyekuwa mwandani wake, Bond Suleiman baada ya kupatwa na kile
kinachosemwa kuwa ni kupandisha majini.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kupandisha
majini hayo kulitokana na jinsi ambavyo mwanaume huyo amekuwa akimtendea
mpenziwe huyo, ambaye inadaiwa katika kupandisha huko, alitoa maelekezo
ya namna anavyotakiwa kufanya.
“Nakuambia ilikuwa varangati siku hiyo,
Wastara alipandisha majini akiwa na Bond, walikuwa wakijaribu kutatua
mgogoro wao, lakini katika hali ya kushangaza, ghafla Wastara
alibadilika na kuanza kusema hivyo kwa sauti tofautitofauti, kabla ya
kumshushia kipigo,” kilisema chanzo chetu, kilichoomba hifadhi ya jina
lake.
Wastara alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo
alimtaka mwandishi wetu kuwasiliana na Bond, huku akidai hata kama ni
kweli, hayo yanabaki kuwa maisha yao.
Kwa upande wake, Bond alikiri kutokea
kwa sakata hilo na hadi wakati huo (Alhamisi) alikuwa Saadan, Bagamoyo
katika Sober House akikamilisha zoezi la kupewa ushauri nasaha.
“Ni kweli niko huku, natekeleza adhabu
niliyopewa na Wastara, ikiwemo kunyoa nywele, kupewa ushauri wa jinsi ya
kuishi. Nimeachana na pombe, mirungi, shisha, kubadilisha wanawake na
starehe nyingine za aina hiyo, sasa nimebadilika, sitamuumiza tena
Wastara, zimebaki siku kama 6 nikamilishe zoezi hili,” alisema Bond.
CHANZO: GPL

Post a Comment