MWENYEKITI WA CHADEMA GEITA AUAWA...Freeman Mbowe amesema chama kimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa hizo
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo enzi za uhai wake. 
Alphonce Mawazo alipokimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Geita kabla ya kukumbwa na mauti.
Katoro, Geita
Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe amesema chama kimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Geita na Mgombea Ubunge Jimbo la Busanda Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo ambaye ameuwawa leo huko Katoro, Busanda.
Kwa niaba ya viongozi na wanachama wote wa CHADEMA, Mwenyekiti Mbowe ametuma salaam za pole na rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, wanachama wa CHADEMA na wote walioguswa na kifo hicho cha kikatili, akivitaka Vyombo vya Dola vitoe taarifa kamili ya wahusika wa unyama huo.
Mwenyekiti Mbowe amemwelezea Mawazo kwama mmoja wa wapiganaji jasiri na makini ambao Watanzania wapenda mabadiliko walikuwa wakijivunia kuwa naye.
"Hakika tumepoteza moja ya nguzo muhimu za chama Kanda ya Ziwa. Chama kimepokea kwa mshtuko mkubwa kifo hiki ambacho tunaamini kimepangwa."
"Tunavitaka vyombo vya dola vitupe taarifa kamili ya wahusika wa unyama huu. Nawapa pole Wanachadema wote, ndugu na jamaa," amesema Mwenyekiti Mbowe akiomboleza kifo hicho.
Mbali ya kuwa Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Geita, Mawazo pia alikuwa Mjumbe wa Baraza Kuu, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Taifa.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mawazo mahali pema. Amina.
Imetolewa leo Jumamosi, Novemba 14, 2015 na;
Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Post a Comment