Hata kama ni ‘used’, Johari ana thamani yake
NENO! Mwigizaji mkongwe kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ameweka wazi kwamba wasanii wengi wachanga wamekuwa wakipenda kutumia jina la ‘used’ kwa wasanii wakongwe lakini kwa upande wake anajiona bado ana thamani kubwa.
Johari ameliambia Ijumaa Wikienda kwamba, japokuwa wanamuita ‘used’ lakini akisimama katika kucheza filamu, thamani yake inakuwa ni kubwa kwani kile anachokifanya anakifahamu vyema wala hawezi kutetereka.
“Sawa, mimi ni ‘used’ lakini thamani yangu ni kubwa sana kwenye Sanaa kwa sababu mimi ni tofauti kabisa na hata methali zinasema ya kale ni dhahabu,” alisema Johari.
Post a Comment