Gwajima, Flora kumlipa mamilioni Mbasha!
Mwimbaji nyota wa muziki wa Injili Bongo, Flora Mbasha.
Stori: Mayasa Mariwata
MCHUNGAJI
Kongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na mwimbaji
nyota wa muziki wa Injili Bongo, Flora Mbasha watalazimika kumlipa
mamilioni ya shilingi Emmanuel Mbasha (33) kwa kitendo chao cha
kumchafulia jina mbele ya jamii, Risasi Mchanganyiko limeelezwa.
Hivi
karibuni, Emmanuel ambaye ni mume wa Flora, alishinda kesi ya ubakaji
iliyofunguliwa dhidi yake katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar
akidaiwa kumbaka mdogo wa mkewe waliyekuwa wakiishi naye nyumbani kwao,
Tabata, Dar es Salaam, Juni 2014.
Katika
shauri hilo, Mbasha alishitakiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(mlalamikaji anakuwa shahidi), kitu kinachoibua maswali ni kwa namna
gani Gwajima na Flora watahusishwa.
GWAJIMA, FLORA WANAHUSIKAJE?
Akizungumza
na Risasi Mchanganyiko jijini Dar juzi, Mwanasheria na Ofisa wa
Mahakama Kuu, Denis Maringo alisema mazingira ya kesi hiyo iliyokuwa
gumzo kubwa, yanawaingiza wawili hao katika madai ambayo Mbasha anaweza
kufungua kwani kuna uhusiano unaojitosheleza kati yao na binti anayedai
kubakwa.
“Inafahamika
kwamba aliyedai kubakwa ni mdogo wake Flora na kwa kipindi chote kile
cha kesi, inafahamika pia kuwa Flora alikuwa karibu na Mchungaji
Gwajima, maana mara nyingi zilisikika kauli za Mbasha kulalamika nyendo
za mchungaji na mkewe.
“Kuna
wakati Mbasha alidai kuwa, alikwenda kwa Mchungaji Gwajima ili kupata
muafaka wa tatizo lake na mkewe, lakini akasema kiongozi huyo wa kiroho
alimwambia kama mkewe ameshaamua, ni vizuri akaheshimu uamuzi wake. Hii
inaonesha ukaribu wa wawili hao,” alisema mwanasheria huyo.
KWA NINI MBASHA ASHITAKI?
Mwanasheria
huyo alisema kuwa, Mbasha anaweza kufungua shauri la madai na kuomba
fidia ya mamilioni ya fedha kutokana na heshima yake kwa jamii kushuka
na kuchafuka, hasa kwa kulinganisha na umaarufu alionao katika jamii.
“Kesi
ya ubakaji inamshushia mtu thamani katika jamii, hivyo kutokana na adha
hiyo, pale unapokutwa huna hatia na mahakama unaruhusiwa kufungua kesi
ya madai kwa lengo la kutaka fidia kiasi unachokitaka na mahakama
kukitolea uamuzi kwa kumshitaki mhusika na wote walioshiriki katika kesi
hiyo.
“Anachopaswa
kufanya Mbasha ni kwenda Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es
Salaam ambayo ni tofauti na ile ya awali iliyoendesha mashitaka na
kufungua kesi ya madai ambapo sheria ya mwaka 1971 inaruhusu mtu
kufungua kesi ya aina hiyo kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu tangu
hukumu itolewe. Kwa sababu ya kudhalilishwa, atawashitaki waliomshitaki
mwanzo kwa kesi ya jinai.”
SHERIA INASEMAJE?
Wakili
huyo alichambua vipengele vinavyompa urahisi Mbasha wa kufungua kesi
hiyo kuwa ni kile kinachohusu nia mbaya ya mfungua kesi akiwa na lengo
la kumchafua.
“Mtu
akikufungulia kesi kwa nia mbaya ya kukuchafua wewe. Kwa hiyo, yeye na
walioshirikiana naye, wote wanahusika. Kipengele kingine ni kile cha
adha ya kuwekwa ndani. Kwa kuwa mahakama ilimkuta hana hatia, maana yake
ni kwamba, kitendo cha kuwekwa ndani ni cha uonevu unaoweza kuwaingiza
matatani hata polisi wenyewe.
“Jambo
lingine linalompa nafasi Mbasha ya kufungua madai ni kwa kitendo cha
jamii kumuona tofauti kiasi kwamba inaweza kumtenga kwa kuamini ni
mbakaji. Ili kuwa fundisho kwa watu wengine, anayo haki ya kudai fidia
kwa kuchafuliwa jina kwani huenda hiyo iliwafanya wahusika kunufaika kwa
dhamira zao.”
Wakati
ishu hiyo ikionekana kuwakalia vibaya Mchungaji Gwajima na Flora,
gazeti hili lilimtafuta Mbasha ambaye baada ya kuelezwa kuhusu
maelekezo ya mwanasheria huyo, aliomba muda wa kutafakari pamoja na
wanasheria wake.
“Ni
kitu kipya unanieleza na kama unavyojua hili ni suala la kisheria.
Siwezi kulitolea maelezo mara moja, inabidi kukutana na kushauriana na
wanasheria wangu ili kuona nini tunaweza kufanya,” alisema Mbasha.
Flora
na Gwajima nao walitafutwa kupitia simu zao za mkononi, lakini mara
zote hazikuweza kupatikana hadi gazeti hili lilipokwenda mtamboni. Hata
hivyo, jitihada za kuwatafuta bado zinaendelea.




Post a Comment