Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.
BAADA ya hivi karibuni wasanii wa filamu waliokuwa
wapenzi, Wastara Juma na Bond Suleiman kutengana, Lulu Semagongo ‘Aunty
Lulu’ ameibuka na kumshauri staa huyo kukubaliana na matokeo.
Aunty Lulu aliyewahi kuwa mpenzi wa Bond, alimtaka mwenzake
kukubaliana na matokeo kwani huenda muda ndiyo umefika na katika
mapenzi, hilo ni jambo la kawaida.

“Sina
la kuzungumza juu ya Bond maana sihusiani naye, mapenzi yalikuwa zamani
ila kama uchumba umevunjika basi namshauri Wastara akubaliane tu na
matokeo kwani hata mimi muda wangu uliisha, tukaachana naye inawezekana
ni hivyo umekwisha pia,” alisema Aunty Lulu.
Post a Comment