Barua kwa kwa watumishi wa umma
Nawasalimuni
nyote katika jina la nchi yetu nzuri Tanzania,
Jina
ambalo huko nyuma sote tuliliimba “Tazama ramani utaona nchi nzuri, yenye mito
na mabonde mengi ya nafaka…nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaa!”
Hakika
wimbo huu vijana wengi siku hizi wanashindwa kuuimba, kwa nini? Uzuri wa taifa lao haupo tena, umepotezwa na
baadhi yenu watumishi wa umma
wasio
na uadilifu.
Sio
siri vijana wetu kwa muda mrefu wameshindwa kujivunia taifa lao, wameshindwa
kuongea mbele za watu kwa sauti kubwa kwamba wao ni Watanzania,
uzuri
wa taifa lao na sifa nzuri ya nchi yao imeharibiwa na vitendo kama ufisadi
uliokithiri ambao umesababisha wachache katika taifa kunufaika huku wengi
wakiteseka.
Ndugu
zangu watumishi wa umma,
Ni kwa
kupitia jina la nchi hii ndiyo leo nawaandikieni, kuwakumbusha juu ya wajibu
wenu ambao kwa muda mrefu sana umekuwa hautimizwi ipasavyo!
Kwanza
kabisa niseme wazi kwamba nayafahamu mateso yenu, nayafahamu mahangaiko yenu ya
maisha magumu, ambayo wakati mwingine yamefanya
uaminifu
wenu kutikiswa.
Pamoja
na hayo yote nasema hakuna jambo hata moja linalohalalisha kwenu ninyi kupoteza
vigezo vitano muhimu vya utumishi wa umma ambavyo ni;
1.UADILIFU
2.UAMINIFU
3.KUSEMA
KWELI DAIMA
4.UZALENDO
NA DHAMIRA
5.HOFU
YA MUNGU.
Yeyote
kati yenu aliyehalalisha kuondoka kwa vitu vitano nilivyovitaja hapo juu kwa
sababu ya aidha kipato kidogo anachokipata serikalini, akavunjika moyo na
kuacha
kuwatumikia wananchi, ama akachagua kuendeleza rushwa na kukosa uzalendo, huyu
hatufai kuwa mtumishi wa umma. Kwa muda mrefu mmekuwa
mkilalamikiwa,
mkinung’unikiwa na wananchi kwa sababu ya utendaji mbovu unaosababishwa na
kukosekana kwa mambo matano niliyoyataja hapo juu,
kwa
kweli ilionekana kana kwamba uadilifu katika taifa hili hauwezekani tena, vivyo
hivyo uaminifu, kusema kweli, uzalendo na hofu ya Mungu vilitoweka.
Uchaguzi
uliofanyika Oktoba 25, 2015 na kumwingiza madarakani rais ambaye hawezi
kumaliza hotuba yake bila kusema “TUNAMTANGULIZA MUNGU
MBELE”
Dk. John Pombe Joseph Magufuli umerejesha tena imani ya Watanzania kwamba,
kumbe utumishi wa umma uliotukuka unawezekana, yote haya
yamefanyika
ndani ya siku chini ya arobaini tangu aingie madarakani!
Kwa
matendo yake hayo, nimesikia kwa masikio yangu watu waliompinga Rais Dk.
Magufuli wakati wa kampeni wakijuta na kusema: “Laiti ningejua
ningempa
kura yangu!” haya yanatokea ndani ya siku chini ya hamsini tangu rais huyu
aingie madarakani, upepo umebadilika, utumishi wa umma uliowekwa
madarakani
na watu kwa ajili ya watu kumbe unawezekana. Ule msemo wa wazungu usemao “Once
you shake the top, you have shaken the bottom” yaani
ukishatikisa
juu, tayari utakuwa umetikisa na chini, sasa umedhihirika kwamba ni kweli. Tanzania inakimbia mbio, kuanzia
serikalini mpaka kwenye sekta
binafsi,
adui uvivu ameanza kupotea kwa sababu tu raia aliyeingia madarakani sio mvivu.
Kwa
mara ya kwanza maishani mwangu nimeanza kusikiliza taarifa za habari na kusikia
habari za kamatakamata, fukuzafukuza, kila kona ya nchi. kila
kiongozi,
kila mtendaji sasa anajaribu kutimiza wajibu wake, yote haya kwa sababu
amebadilishwa mtu mmoja tu juu ambaye kauli mbio yake ni “HAPA KAZI
TU!”
Ndugu
zangu Watumishi wa Umma,
Nawaandikieni
barua hii kuwakumbusha kwamba ile kauli yenu ya kusema “huu ni moto wa mabua”
naomba muiache, anayesema hivyo hamfahamu vizuri
rais
wetu, kwa wanaomfahamu hawawezi hata siku moja kutoa kauli hiyo, haigizi, haya
ndiyo maisha yake, ni kama mapafu ambavyo kazi yake ni kupumua,
ndiyo
ilivyo kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Ndugu
zangu,
Nawasihi
mfanye kazi, timizeni wajibu wenu mliopangiwa kwa faida ya taifa hili, ambaye
hatayasikia maneno haya, hakika ajiandae kukumbuka ninachokisema
kwani
mfumo utamtema! Ni wakati wa kuchapa kazi, si wa kuchati kwenye mitandao ya
jamii saa ya kazi. Tukifanya jambo hili
kwa pamoja, ninawahakikishieni
taifa
letu litasonga mbele kutoka hapa tulipo kwenda tunakotakiwa kwenda, rais wetu
ni MUADILIFU, ndivyo itakavyokuwa kwa Makamu wake wa Rais Samia
Suluhu
Hassan, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, serikali nzima na hatimaye
vijijini, vivyo hivyo katika uchapakazi, kama rais wetu si mvivu, wavivu
wote watang’oka,
watake wasitake.
Matarajio
yangu ni kwamba kama watumishi wa umma mtatimiza vyema wajibu wenu, mtafanya
kazi kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo wa hali ya juu,
lazima
kipato cha taifa letu kitaongezeka na maisha yenu yataboreshwa na rais huyu huyu
tuliyemweka madarakani. Lakini niwasihi
msipoteze hali yenu
ya
kujiamini kwa kusema “Rais ni mkali mno” matokeo yake mkawa ni watu wa
kutekeleza mambo kwa nidhamu ya woga, taifa la watu wenye aina hii ya
nidhamu,
ambao hutekeleza mambo yao kwa kutaka tu kumfurahisha mkuu huwa halisongi
mbele, matokeo yake huzaa hata uonevu kwa sababu tu mtu
alikuwa
anataka aonekane anafanya kazi.
Sidhani
rais wetu ni mtu wa aina hii, bali ni mtu anayependa kufanya kazi na watu
wanaojiamini na wachapakazi na atakuwa tayari kujenga jamii ya watu wenye
kujiamini
si wanaotetemeka ovyo kila wanapokutana naye wakimpa ushauri anaopenda kuusikia, si ule anaotakiwa
kuusikia hata kama hautamfurahisha.
Nimeyasema
haya kwa sababu msipokuwa makini wale mlioko madarakani, wakuu wa mikoa, wakuu
wa wilaya, wakurugenzi nk. Mtajikuta mkionea watu au
kuwatoa
watu sadaka kwa sababu tu mnataka kumfurahisha mkuu au muonekane mnafanya kazi
na baadaye kupanda vyeo kwa gharama za maisha ya watu
wengine.
Sitaki
kusema mengi siku ya leo, kwa haya machache niliyoyasema nawatakieni utendaji
mwema wa kazi katika Awamu hii ya tano ya HAPA KAZI TU! Tendeni
kazi
zenu kwa kujiamini na uadilifu wa hali ya juu, nawahikikisheni awamu hii ya
tano itabadilisha maisha yenu, kama anavyosema mwenyewe Rais Magufuli,
tumuombee
kwa Mungu atimize ndoto yake yakutufikisha kwenye nchi ya ahadi.
Ahsanteni.
NUKUU
WASALAAM
Eric
Shigongo James
Post a Comment