ad

ad

Alichosema Aliyekuwa mgombea ubunge wa CUF jimbo la Namtumbo - Bonifasia Mapunda



NIMETHUBUTU,NIMEWEZA ,NASONGA MBELE, ASANTENI WOTE.
Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu,mwingi Wa rehema kwa afya na uzima anaonipa mpk sasa.Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kwa kuwa nami akinipigania usiku na mchana katika kipindi chote cha kampeni .Nipende kuchukua fursa hii kuwashukuru Chama cha wananchi CUF kwa kuniamini na kunipa dhamana ya kuwa mgombea Wa jimbo la Namtumbo,Pamoja na dhamana mliyonipa bado nawashukuru kwa support yenu ya Hali na Mali mliyonipa hususani ofisi ya Katibu Mkuu chini ya Mheshimiwa Maalim Seif .Pia Nitoe shukrani zangu toka ndani ya moyo Wangu kwa Mkurugenzi Wetu Wa uchaguzi Mhe Shaweji Mketo na timu yake yote ya uchaguzi kwa kazi kubwa mliyoifanya katika kunipigania.Shukrani zangu za pekee zimuuendee baba na mama Yangu mzazi kwa kuniunga mkono kwa asilimia zote na kunisaidia kwa hali na Mali kipindi chote nilichokuwa kwenye mapambano.,Mama Yangu wewe ni mama ambaye najivunia kuwa na mama wewe kwenye maisha Yangu .Umenipigania sana asante mama Bonny.Nitakuwa mchoyo Wa fadhira nisiposema asante kwa uongozi Wa CUF na CHADEMA (UKAWA)wilaya ya Namtumbo kwa kazi kubwa walioifanya kipindi chote cha kampeni. Nashukuru timu Yangu ya kampeni pia.shukrani zangu pia za pekee ziende kwa marafiki na ndugu zangu waliojitoa kwa ajili Yangu kwa uchache nimtaje Julius Mtatiro,Agnes Nkwera,Nurubico Mponda, Asteria Shao,Tumaini ,Merk Mapunda na Deus Kapinga.Mwisho niwahukuru Wananchi woteee Wa Jimbo La Namtumbo mlinionesha upendo Wa ajabu kwa kunipokea kwa mikono miwili sitawasahau wale wote waliokuwa wakivua mashati na kanga zao kutandika barabarani ili nipite,Kura hazikutosha sana ijapokuwa tumechakachuliwa sana niseme ASANTE tujipange for 2020
Aluta continue......
Bonifasia Mapunda
0786484343
Powered by Blogger.