Wavuvi watakiwa kuhakikisha wanakuwa na vibali vinavyowaruhusu kuendesha shughuli hizo
Tahadhari imetolewa kwa baadhi ya wavuvi wakubwa wa ndani na wa nje wanaoendesha shughuli za uvuvi katika baahari kuu ya Tanzania bila ya kibali kuhakikisha wanakuwa na vibali vinavyowaruhusu kuendesha shughuli hizo ikiwa ni pamoja na kulipa kodi inayostahili kwa serikali kwa kuwa serikali ijayo ya awamu ya tano chini ya Dr John Pombe Magufuli haitakubali eneo la bahari la Tanzania kugeuzwa shamba la bibi.
Tahadhari hiyo imetolewa na mgombea urais wa chama cha mapinduzi Dr
John Pombe Magufuli wakati akizungumza na wananchi wa Kilwa Masoko
mkoani Lindi na kuwaeleza kuwa serikali ijayo itahakikisha inaboresha
shughuli za uvuvi kwa wavuvi wadogowadgo ikiwa ni pamoja na kuwapatia
mikopo ili waweze kuinuka kiuchumi na kuonya serikali yake haitavumilia
shughuli za uvuvi haramu hasa unaoendeshwa na wavuvi wakubwa katika
bahari kuu ya Tanzania huku
serikali ikipoteza mapato.
Pia mgombea huyo wa urais wa CCM Dr John Pombe Magufuli amewataka watendaji wa serikali yake ya awamu ya tano kujipanga kuwatumikia wananchi hasa wa hali ya chini na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Akitokea mkoani Lindi alikofanya mikutano ya kampeni takribani saba
na kuingia mkoani Pwani safari iliyokuwa ikichelewa kwenda kwa wakati
kutokana na mapenzi ya wananchi kwa Dr Magufuli kumsimamisha mara kwa
mara barabarani ambapo baadhi ya wananchi wa wilaya ya Rufiji katika
eneo la Kibiti wameelezea changamoto zinazowakabili huku wakimtaka Dr
Magufuli atakapoingia madarakani kutekeleza ahadi iliyotolewa na Dr
Jakaya Kikwete ya kujenga kwa lami barabara inayoelekea katika hospitali
ya Mchukwi ili kuondoa changamoto ya usafiri kwa wagonjwa wanaokwenda
kupata tiba katika hospitali hiyo.



Post a Comment